Kenyatta Mayanga
Mke wa Kenyatta, Juliana Morris, Mwinyikheri Mkwazi, Jabir Jongo, Kruu nzima ya wanakijiwe cha ughaibuni inatoa shukurani kwa wale wote waliochangia kwa aina moja au nyingine kwa lengo la kumsaidia ndugu yetu, kaka yetu Kenyatta Mayanga anayeshikiliwa na uhamiaji kwa sasa. Pesa iliyokusanywa mpaka sasa hizi ni $2,500/- na ambayo mwanasheria aishapewa bado $2,500/- aanze kazi ya kumtoa ndugu yetu Kenyatta.
Mwanasheria huyu ndio mwanasheria wa Kenyatta tangia mwanzo na ndiye mwenye majarida yote ya Kenyatta kwa hiyo tunashukuru kwa mtoa wazo la kuangalia uwezekano wa wanasheria wengine.
Michango bado inahitajika ili kuweza kumalizia nusu iliyobaki na wakili wa Kenyatta aanze kazi yake ya kumtetea ndugu yetu.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Juliana Maorris 781 354 2983 Jabir Jongo 240 604 0574 au Mwinykheri Mkwavi 240 603 3274
Tunatanguliza shukurani
No comments:
Post a Comment