Mkuu
wa mkoa wa iringa DK CHRISTIN ISHENGOMA amewataka wananchi mkoani
Iringa,kutokuwa na hofu katika kipindi hiki cha kuelekea kampeni za
uchaguzi wa jimbo la kalenga.
Akizungumza leo kwenye
moja ya kituo cha redio mjini humo,Nuru FM ,kupitia kipindi cha
sunrisepower, amesema kuwa tayari ameshakaa na kamati yake ya Ulinzi na
Usalama akiwemo Kamanda wa Jeshi
la Polisi,aidha ameongeza kuwa wamejiandaa kikamilifu katika ulinzi,
hivyo wananchi
wanapaswa kutokuwa na hofu.
Amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa jimbo
hilo wageni wengi watakuwa wanaingia hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na
vishawishi vya makundi mabalimbali katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuwa yeye yupo
katika vikao vya bunge maalum la katiba atakuwa anakuja kushiriki na wananchi
katika mkoa wake katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kampeni zinazoendelea.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kuhusu suala la posho
kwa upande wake yupo tayari kupokea kiwango chochote atakachopewa ambacho kitakuwa
kinatolewa katika kikao cha bunge maalum la katiba.
No comments:
Post a Comment