Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wanachuo.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana
kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa
mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa
wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa
mwizi.
Wanachuo wakikagua baadhi ya
vitu alivyokutwa navyo Emmanuel.
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku
watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu,
wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo,
sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya
kukamatwa kwa jamaa huyo.
Emmanuel akiwa mikononi mwa wanachuo wenye hasira.
Wanachuo hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na
kumwachisha Emmanuel udokozi, walikuwa wakimhoji maswali huku
wakimwangushia kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu
nyingi iliyotapaa sakafuni kama buchani.
Emmanuel akiwa na vitu vya wizi alivyokutwa navyo.
Kama kawaida, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia kuangalia
kipigo tu, waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda
waliomuona jamaa huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa.
“Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.
Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama ghafla, nikashtuka
lakini sikutaka kuwa na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,”
alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na
kuendelea:
“Nikaondoka hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa
mzito, ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi.
Nilipofika mapokezi, yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza
kumtafuta, nikaona akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo
ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka
alipokamatwa,” alisema Adolphina.
Jamaa huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na
vyeti mbalimbali vya shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha
kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake.
Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM
zikiwepo za CRDB, NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia
kwa ajili ya kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.
Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya
Huawei yenye thamani ya shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya
shilingi 150,000, ambazo zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache
zilizopita.
Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo
walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la
tukio baada ya kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo
akisulubiwa kwa hasira
NA GPL
No comments:
Post a Comment