ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 1, 2014

SIRI 7 ZA KUVUNJA NDOA NA MBUNGE BIBI HIZI HAPA

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.

Stori: Imelda Mtema na Ojuku Abraham
YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.

Michael Christian‘hendsam’boi’ aliyevunja ndoa na ndoa hiyo na mheshimiwa huyo ndani ya Ofisi za Global.

SIRI YA KWANZA
Kijana Michael aliianika siri ya kwanza kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima. 

SIRI YA PILI
Akizungumza kwa hisia kali, Michael aliye na taaluma ya uuguzi, aliiweka wazi siri ya pili ya kuamua kuivunja ndoa yake na mheshimiwa huyo kuwa ni kitendo cha kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka.
Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.
SIRI YA TATU
Kijana huyo aliendelea kwa kuifunua siri ya tatu kuwa ni kitendo cha kufungishwa ndoa bila kuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui. 

SIRI YA NNE
Siri zilizidi kubanjuliwa, Michael alisema sababu ya nne ambayo pia ilimsukuma kuamua kubatilisha ndoa yake na mama Kasikila ni baada ya kubaini kwamba, hataweza kupata uzao kwa mke huyo kwa sababu ana watoto wakubwa kiumri kuliko yeye.
“Nilijua sitapata watoto, hakukubali kuzaa na mimi kwa sababu tayari ana watoto wakubwa, mimi mdogo, ingekuwa vigumu. Kifupi haikuwa ndoa halali kwangu,” alisema kijana huyo.

SIRI YA TANO
Michael: “Alianza kunibana sana, kila hatua ya miguu yangu alitaka kujua inakwenda mpaka wapi! Hii hali nikaiona inanipiga pingu, nikagundua kuwa kumbe mimi sijaoa, bali nimeolewa. Yule mama alinioa mimi, si kwamba mimi nilimuoa yeye, nikasema ili niwe na amani ya moyo ni lazima ndoa ivunjike.”

SIRI YA SITA
Kijana huyo hakuona sababu ya kubakiza siri hata moja, akaendelea kuzianika:
“Jambo jingine ambalo pia lilichangia kuamua kuivunja ndoa ile ni baada ya kukumbuka historia ya kukutana kwetu. 
“Wakati nipo Hospitali ya Bagamoyo na yeye akiwa pale kama muuguzi mkuu, tulizoeana. Kuna siku aliniita kwake akasema anasafiri anaomba nimwangalizie nyumba, nilikuwa na rafiki yangu tukawa tunalala pale mpaka aliporudi. 
“Kuzoeana kuliendelea, mwishowe tukawa wapenzi mpaka ndoa. Nilipokumbuka hivyo tu nikagundua kuwa aliniingiza mapenzini kwa hila au mbinu, hilo pia sikulipenda,” alisema Michael. 

SIRI YA SABA
Michael alisema sababu ya saba ambayo pia ilimshinikiza kuivunja ndoa hiyo ni kupwaya ndani ya nyumba.
Alisema kutokana na umri wake, ndani ya nyumba alijiona ni mtoto na si mume kama wanaume wengine walivyo.
“Hata uwezo wangu wa mawazo kwake haukuwa wa mume na mke, ni wa mtoto na mama. Kifupi haikuwa ndoa halali,” alisema.

SIKU ALIPOIVUNJA NDOA
Kijana huyo alisema ndoa yake na mheshimiwa huyo aliivunja mbele ya Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare walipokwenda kusuluhishwa ili waende wakaishi kwa amani. 
Alisema kabla ya usuluhishi alimfungukia mama Rwakatare kuhusu manyanyaso anayoyapata ndani ya ndoa hiyo ndipo aliposimama na kuivua pete kisha kuitupa chini huku akisema katu hawezi kurudi kwa mkewe huyo na ndoa imevunjika, akaondoka zake.

ANATAKA KILIO CHAKE KIFIKE KWA JK
Kijana Michael alisema kilio chake kikubwa kwa sasa ambacho angependa kifike hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ni kitendo cha mkewe huyo kuzuia vyeti vyake ambavyo vingemsaidia kutafutia kazi sehemu mbalimbali.

“Amezuia vyeti vyangu vyote, kila nikimwambia navitaka nikienda ananifanyia visa, nawaomba Watanzania wanisaidie kwa hili.
“Mimi kwa sasa nataka vyeti tu, sitaki cha ndoa wala nini? Lakini hataki kunipa,” alisema Michael.

MSIKIE MBUNGE SASA
Akijibu tuhuma hizo, Mheshimiwa Kasikila alikiri kuwa na vyeti vinavyolalamikiwa na mumewe huyo, lakini alikanusha kwa nguvu zote juu ya maneno kuwa yeye ameoana na mtoto mdogo, akirejea vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyomtaja mtoto kama ni mtu wa namna gani.
Mbunge: “Mwandishi, unafahamu mtoto kwa katiba yetu ni mtu wa namna gani?”
Mwandishi: “Ni mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.”
Mbunge: “Sasa Michael ni mtoto? Ana miaka 28 unamuita mtoto?”

AWAWEWESEKEA WANASIASA
Alisema anajua suala hilo lina shinikizo la kisiasa, kwani hivi karibuni baadhi ya wanasiasa walikwenda jimboni kwake wakiwa na nakala ya gazeti moja lililoandika habari zake na kijana huyo na kuwaambia wapigakura wake kuwa mbunge wao ameoa kitoto, lakini wapigakura wake waliwapuuza kwa kuwaambia hilo haliwahusu kwani wanachojua anawawakilisha vizuri bungeni.
“Kama kweli ninyi mnampenda huyo Michael, muelekezeni sehemu sahihi ya kwenda kupeleka madai yake. Ngoja nikupe mfano, mimi nikiwa wizara ya afya, mtu akija na malalamiko kuhusu pembejeo za kilimo, kwa kumsaidia, nitamuelekeza aende wizara ya kilimo, kwa kuwa pale (afya) siyo sehemu yake, sasa nyinyi muelekezeni huyo sehemu sahihi ya kupata haki yake, siyo huko magazetini,” alisema mama huyo.

MAMA RWAKATARE BWANA
Kwa upande wake, Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kwa lengo la kumsikia chochote kuhusu ishu hiyo, alianza kulalamikia habari iliyoandikwa miezi miwili nyuma na kukata simu.
GREDIT:GPL

19 comments:

Anonymous said...

nakubaliana asili mia 89 na mama rwakatare kwa maneno yake.Dogo handsome boy Michael christian naona kama ameshukumwa kwa mvuto wa kisiasa na siku hii bongo kuna style ya kuchafuana mtu ukiwana beef na mwenzako vyovyote vile tena mwenzaka akiwa na hadhi kama cheo serikalini,mfanyabiashara maarufu au cheo chochote kile ambacho anajulikana mtu basi cha kufanya ni kwenda kwenye magazetini na kumchafulia hii tusipingie ipo sana hapa kwetu nyumbania tanzania ni mambo mambaya sana haya na wandishi kushindwa kutekeleza uandishi wao

nchi za wenzetu zipo hizi lakini ukijitoa hivi ujue kama unasema uongo au kwa chuki zako basi ujue mwenzio anaweza pia kukufungulia mashitaka.

na maswali mawili matatu dogo michael christian ulikuwa hujui kama unapofunga ndoa hiyo kwamba wewe utakuwa umeolewa?
kiumri,kifikra na hata cheo kwa vile pesa anazo mama na pia katika experience kimaisha.

je bado unajiona dogo na sheria inasema kwamba miaka 18 ndo mdogo.

sema tu ulichokuwa nacho rohoni dogo na wengi vijana wakiume ndo hivyo tena wanatafuta yao wakikosa au wakidanganywa na wanasiasa basi wanaona bora tutoke kule kwenye siasa nitapata zaidi.

tamaa mbaya dogo na wadogo wote wa kiume na kike wenye kupenda watu waliowazidi umri si vibaya mapenzi hayana chaguo lakini wengi wenu mnajiingiza ili mpate chochote tamaa mbaya kitu cha bure always kita ku COST kaeni na kuzingatiye hilo mkipenda ufahari na vya bure bure na kubweteka MTAPAKATWA WATOTO WA KIUME halafu mnakuja kwenye magazeti mkidhani mnawachafuli kumbe unajidhalilisha mwenyewe.

sharobaro mzima kidume cha mbegu ulikuwa unafikiria nini kama si dezo dezo halafu eti sasa unajidai kulalamika ulivyovikosa vya dezo ujue watu wanavihangaikia na unapopewa usione kwamba vya bure bure ita ku COST.

USIRUDIYE TENA KAMA KWELI HUPENDI VYA BURE MNATULETEA USANII WENU HAPA.

Anonymous said...

dogo wote wakike na wakiume wao wanapenda siku hizi masugar mummy na daddy kwao wao mtaji ni viuno, kiuno mtaji so usilalamike kadogo kadogo kaza puti tafuta solution upate vyeti vyako nashauri bora umbebeleza maamsap atakupa vyeti na si eti kuja katika magazeti kumchafulia hasaidi ndo kwanza atakuwa mbogo bembeleza bwana atakupa vyeti vyako ikishindikana nenda ukapate vyoto copy ya vyeti vyako kama original huna.

pole sana kadogo kadogo ni fundisho hili lakupenda dezo dezo za kupakatwa pole sana

Anonymous said...

hasira ya mwanamkee si mnaiona the power of a woman mama mbuge nimefurahi kwa maneno yako poa ngangari mamaaa msikishe adabu ka handsomeboy

Anonymous said...

Punda wewe ulipomuoa mtu Kama bibi yako ulitegemea ninii? Tamaa tu inakusumbua Mimi nilitaka akuchape kwa bakora. Shwain

Anonymous said...

Tamaa, vya dezo , aibu kwa wote walioolewa na watu wazima!!!tafuteni riziki zenu,mnadharauliwa mno. Hizi tabia mbaya zinawadhalilisha wengi, mwisho wao hawapati chochote na kuchafuliwa sifa miaka na miaka.

Anonymous said...

Bwana ee ukichukua sugar mammy au ukichukuliwa na sugar daddy then ukawamwaga outcomes zake ndizo hizi, tena wewe umepewa dozi ndogo hebu mpigie Wema ili akueleze dozi yake ilikuwa cc ngapi.
Halafu mbona unataka kumfanya raisi wa nchi km mjumbe wa nyumba kumi haya ya chumbani yanamahali pake.ie polisi
otherwise huo ndio ukubwa, ulitaka kukwea mbuyu wkt hata muembe huuwezi...

Anonymous said...

SASA NI FUNDISHO WA WALE MNAOTAKA AU MLIOKUWA NA MPANGO KUWA MA-MARIOOO HAPA MAREKANI.

Anonymous said...

Kuhusu kupotea au kutopewa vyet vyako, nenda vyuo ulivyosoma watakueleza vitu vya kufanya ili upate vyeti vyako. Mara nyingi huwa ni kutoa ripoti polisi kuwa vimepotea, kulipia pesa fulani na kuacha chuo kifanye uchunguzi kwa muda fulani halafu wanakupa vyeti vyako.

Anonymous said...

What a stupid excuse? Mtoto wa kiume komaa; acha upumbavu! Kama ulifunga ndoa kwa nia njema, hoja za kutokufuatwa kwa sheria ya ndoa zinapaswa kutolewa na mtu mwingine anayepinga ndoa yenu (SIYO wewe mwanandoa). Ndoa ya kweli inafungwa mioyoni mwa wanandoa SIYO kwa kuwepo cheti halali cha ndoa. Wapo wengi wamependana na wakaishi maisha yao yote kama mume na mke bila exchange ya marriage vows mbele ya kasisi, mchungaji, sheikh, etc. Tuambie ulitaka shortcut ya maisha, lakini mambo hayakwenda sawa na matarajio yako. Who told you there can be a GAIN without a PAIN? Kubali maumivi na uendelee na maisha yako kuliko kuendelea kupoteza muda wako na vyombo vya habari ukitafuta sympathy ambayo si stahili yako.

Anonymous said...

Non story, kama ni kweli basi huyu hendisam boy ni moja ya mahayawani. Yani kwanza uingie kwenye mapenzi, pili uhamie kwa mama wa watu, tatu ufunge nae ndoa...halafu miaka kadhaa baadae uje usingizie utoto kwa tama zako. Hebu kuwa mwanaume don't kiss n tell, na acha kumdhalilisha mama wa watu. By the way u r an idiot, son of a.......

Anonymous said...

"Always short cut is a long cut" jipange Mario's ww,proffesional unayo approved kwann upende slope .....?!

Anonymous said...

jamani kuweni wastaarabu mapenzi hayachagui unaweza kumpenda yeyote yule hata akiwa kibibi kizee na kibabu si wote eti wanataka mteremko na dezo dezo kwa ku fall inlove na mashuggar mummy na daddy.
usiombe yakukute mapenzi si yakufanyiwa mchezo mchezo na kwa nini msimlaumi na huyu mbuge mnamuonea na kumsulubu mtoto wa mwana wa mwenzenu kumbukeni kuna siku yatakuja kukukuteni kupenda hakuchagui dini ragi wala umri mifano ipo chungu nzima duniani so be careful
pole sana bwana mdogo michael christian.pole i feel your pain man.

Anonymous said...

Tukubali tusikubali mwanamke siku zote ni mlezi so nashanga watu wanavyo msema jamaa utadhani kafanya dhambi kubwa gani ambayo hasameheki kuna watu wanayafanya mengi zaidi ya haya tukubaliana ni mfumo wa kidunia every one is looking to survive na anapigana na vita vyake kuna mengi tu majumbani yanatokea kwa mkee na mume na watoto na wazazi mmeleoni hili la ajabu.

Anonymous said...


kuwa ma marioo hapa marekani hata ulimwengu mzima si vibaya kama mama hajali na anakupenda na analipa si ndo life style ya kimarekani wacheki mademu wa kimarekani wanavyo take care their men toka mavazi,malazi, chakula na makazi jamaa kazi yake tu TO MAKE BABIES so whats the big deal mbona hamsemagi wakati mnavyotunzwa na wanaumeee mnakaa kimya na kupenda raha za wanaumme siyo.

Let me tell you this its over now it our time

ma mariooo for ever in america mtaji wangu mimi kiuno na sichoki

kuwa mari00

Anonymous said...

MA MARIOO NDO WAKINA NANI TENA JAMANI TUELIMISHENI SISI WASHAMBA WA KISWAHILI HICHI TAFADHALINI

Anonymous said...

hakuna aibu yeyote ile kuolewa na mtu mzima kwanza wanawake wanaakili sana so nataka nileleewa na mtu mzima kuliko na kicheche chamitaani ukimwambia hivi anakuambia vile ya nini chunguzeni mtakuja kujua faida ya kuwa na mpenzi mtu mzima anakupa mapenzi ya kweli hayana longo longo na cha pili atakuwa na wivu sana na wewe lakini ukijua kumtuliza inakuwa kama kumsukuma mevi mlenda na sukuma wiki inateleza rohoni baridi ugari wako unatua tumboni mwaaaaa

watu wazima dawa nawashauri wote muwe na wapenzi watu wazima vitoto visichana na vivulana vidogo dogo mnapoteza time zenu nao hakuna life,life ipo kwa watu wazima na ndoa inadumu kama huna tamaa ka kijinga jinga

Anonymous said...

wanaume wengi siku hizi wanapenda kuwa ma marioo kwa ugumu wa maisha na kukwepa majukumu yao ukimpata mwanamme wa kweli anayekupenda na kukutumza na kukujali na kukuheshimu usimuache na msukuru mungu sana.
lakin wako wapi hawa wanaumme wa kweli katika karne hiii????

Wanataka mwanamkee awe anawalisha wao na yeye anakaa nyumbani kujibweteka

Anonymous said...

wanaume wa kutaka dezo dezo wako wengi tu na kuwafanya wanawake vidaraja vyao vya kurukia njia safari hii mbona wataumbuka mbugee nimefurahi sana kwa kumpa fundisho kijana huyu wa kiumeee asiye na haya wala kuona vibaaya

Anonymous said...

tuabiyeni waosha vinywa wadau wa hii blog wema sepetu kapewa cc ndozi ngapi? tupasheni udaku tafadhalini mwenye kujua story za wema kubwagwa na sugar daddy wake