Aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Nduli Ayub Mwenda akijinadi mbele
ya mwenyekiti wake Chadema Taifa Freeman Mbowe,katika uchaguzi huo
uliofanyika hivi karibuni mgombea wa CCM alishinda
Wana CCM Nduli wakimpongeza mshindi wa nafasi ya udiwani Bw Mtove ..............................................................................
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com Dar
Kituo
cha taarifa kwa
wananchi (TCIB) kimetoa
tathimini ya uchaguzi
mdogo wa madiwani
uliofanyika hivi karibuni
sehemu mbalimbali nchini , na
kubaini mambo kadha
wa kadha katika
chaguzi hizo ikiwa
ni pamoja na
kampeni hizo kukosa
busara,
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam Mkurugenzi
mtendaji wa TCIB,
Deus Kibamba amesema
kuwa vitendo vya
ukosefu wa busara
wakati wa kampeni
ikihusisha maneno ya
vijembe,shutuma na fujo
za mara kwa
mara , pamoja na
baadhi ya wafuasi
wa vyama kupanda
majukwaani na
kuwashambulia wagombea pinzani
wao kwa kutumia
vyeo vyao katika
vyama, sambamba na
maeneo wanakotoka,Ambapo kibamba
amesema hayo yote
yanachangia kupoteza dhana nzima
ya umuhimu wa
kampeni za kistaarabu
na inachangia pia
kupunguza idadi ya
watu wanaohudhuria mikutano
ya kampeni.
Kibamba
aliendelea kusema kuwa
fujo za mara
kwa mara zimekuwa
zikitokea hasa kipindi
cha kuelekea mwishoni
mwa mikutano ya
kampeni,Ambapo alitolea mfano
katika kata za
Sombetini, Nyasura na Nduli
ambako watu hawakuwa
huru kusema wanaunga
mkono chama gani
kwa kuhofiwa kufanyiwa
fujo na hata
kuharibiwa mali zao, Na
hivyo TCIB kupendekeza
adhabu kali ziwe
zinatolewa kwa wagombea
na mashabiki wanaobainika
kuendesha siasa za
fujo,matusi,kejeli,na dharau ili
kukomesha kampeni chafu.
Aidha
Kibamba amesema kuwa kumekuwa
na baadhi ya
viongozi wa vyama kusikika
wakitoa kauli ambazo
zina dalili ya
kuhamasisha fujo dhidi
ya washindani wao.Hivyo
kutokana na hali
hiyo TCIB imeanza
mawasiliano na Mwendesha
Mashitaka Mkuu wa
Mahakama ya Kimataifa
ya uhalifu wa
dhidi ya binadamu
(ICC) Bi. Fatou Bensouda
kwa lengo la
kumuomba atume timu
ya wataalam wake
kuja Tanzania, ili
kufanya uchunguzi na
tathimini ya awali
juu ya matamshi
ya hivi karibuni
ya Mheshimiwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania, pamoja na
matamshi ya hivi
karibuni pia ya
Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Jakaya
Mrisho Kikwete ambapo
alinukuliwa akiwataka wanachama
wa chama chake
kuacha unyonge na
kuonewa wakati wa
uchaguzi na waamke
na kujibu mapigo.
Ambapo
Kibamba amesema kuwa
endapo matamshi kama
hayo yakiendelea yanaweza
kusababisha fujo kubwa
na kupelekea mauaji
ya ajabu hususani
kuelekea uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015.
Pamoja
na hayo Kibamba
amesema kuwa kumekuwa
na tatizo la
mwitikio mdogo wa
wapiga kura, tatizo
ambalo linaonekana kukua
zaidi na kuwa
tatizo kubwa, Na
kusema kuwa mbaya
zaidi baadhi ya
vyama vimeonekana kufurahia
pindi wanapoona watu
wachache zaidi wakijitokeza
kupiga kura,Hivyo TCIB
imependekeza sheria za uchaguzi
zifanyiwe mabadiliko ili
kuzuia mshindi kutangazwa
mpaka idadi ya
wapiga kura inapofikia
asilimia hamsini ya
wapiga kura walioandikishwa katika
eneo husika.
Sambamba
na hayo Kibamba
amesema kuwa TCIB
imesikitishwa na mwitikio
mdogo wa upigaji
kura pamoja na
kuwepo kwa hamasa
kubwa inayoonekana wakati
wa kampeni.
Na kutokana
na hali hiyo
TCIB ilitaka kujua
tatizo hasa ni
nini, na ndipo
walibaini kuwa uboreshaji
usio wa kudumu
na wa mara
kwa mara wa
daftari la kudumu
la wapiga kura
umekuwa ni tatizo
kubwa linalowakosesha wananchi
wengi haki ya
kupiga kura hususani
vijana waliokuwa na
umri wa miaka
17 wakati wa
zoezi la uboreshaji
wa daftari kwa
mara ya mwisho
mwaka 2010.
Hivyo TCIB
imetoa wito kwa tume
ya uchaguzi kuweka
utaratibu wa watu
kujiandikisha kila mara
na sio mara
moja kila baada
ya miaka mitano.
Halikadharika Kibamba amesema kuwa kutokana na masuala yaliyojitokeza katika tathimini na ufuatiliaji walioufanya wa uchaguzi mdogo wa madiwani,wamegundua ipo haja ya kuimarisha mfumo mzima wa uchaguzi kwa kuweka makatazo juu ya mambo yanayotishia kuharibu uchaguzi, na kuongeza kuwa TCIB ipo tayari kusaidia kuimarisha Jeshi la polisi kwa kuwapeleka kuona jinsi Polisi wa Nchi nyingine wanavyosimamia usalama katika uchaguzi.
No comments:
Post a Comment