Askari akijihami wakati wa vurugu kubwa zilizozuka leo majira ya jioni Jiji la Mombasa wakati Waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti 'Masjid Mussa' ambapo waumini hao wamedaiwa kuwa walikuwa wameandaa mkutano wa hadhara waliouita Kongamano ambao Serikali ilikataa kutokuwepo kwa muhadhara huo na wao kupinga maamuzi hayo.
Imeelezwa kuwa Baada ya kukatazwa kufanya muhadhara huo, waliamua kuweka Bendera ya Kiislamu katika Msikiti huo huku wakitoa 'Fatwa' kuwa kuanzia leo hawaitambui Bendera ya Kenya, jambo ambalo lilipelekea kutokea kwa vurugu hizo baina ya Askari na waumini hao. Aidha imeripotiwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia katika vurugu hizo na wengine kujeruhiwa.
Mmoja kati ya waumini hao akiwa hoi baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo.
Askari wakilinda moja ya mtaa unaoelekea Msikitini hapo.
Taswira ya msikiti huo.
Mmoja wa majeruhi...
Waumini hao wakitolewa msikitini humo baada ya Hambushi ya nguvu,
Credit: Sufiani Mafoto
2 comments:
Hii the greatest economy in the region mbona majanga.wakati ya Al shabab yakiendelea haya mengine tena.
wanafanya wenyewe wanawasingizia waislamu si ndo propaganda za kiulimwengu wanawaogopa waislamu so cha kufanya hawana ila kuwasingizia kila leo kwa matukio maovu kama haya mungu mkubwa lakini yuko nao amen
Post a Comment