Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na viongozi wa
CCM katika kata ya Mgama kijiji cha Mgama mara baada ya kuwasili kjijini
hapo kwa ajili ya kufanya mkutano na wajumbe wa harmashauri kuu ya
Kata hiyo ili kujadili kwa pamoja mwennendo wa kampeni katika jimbo la Kalenga ambapo chama hicho kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wa jimbo hilo, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA)
Kata hiyo ili kujadili kwa pamoja mwennendo wa kampeni katika jimbo la Kalenga ambapo chama hicho kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wa jimbo hilo, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA)
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kuimba wimbo na
wana CCM mara baada ya kuwasili katika kikao hicho cha ndani
kilichofanyika kwenye kijiji cha Mgama.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akishiriki kucheza ngoma
kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa ndani uliofanyika leo kwenye kijiji
Mgama Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifurahia jambo kwa kupiga
makofi wakati wa mkutano huo wa ndani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Iringa
Vijijini mama Delfina Mtavilalu. Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza na waandishi wa
habari kijijini Mgama mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa ndani. Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisoma mambo muhimu yanayohusu uchaguzi huo kwa wana CCM. Baadhi ya viongozi wa CCM katika ngazi ya vijiji na kata wakiwa katika mkutano huo Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula ukiwasili katika kijiji cha Mgama Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisisitiza jambo wakati
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
wa ndani
................................................................................................
MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama cha
CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa
kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.Mangula
amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda uchaguzi
mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini.Kiongozi
huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha Mugama kata ya
Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu
ya CCM ya kata hiyo.
Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM kata
ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho ni
mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda.
Samson
alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya Mugama jambo
linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu chafu ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake. Baada
ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo ndani ya
kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika.
“CHADEMA
hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza kusema kina
dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au wanatakakuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema. Alisema
CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na mafanikio na
utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa.
Kwa
mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa CCM
hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe ahadi
zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi, alisema
Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo hakuna mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo.
Betha
alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi yote
yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi wake siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura. Alisema
viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani
kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili kuhakikisha ubnafanyika kwa amani. Aidha,
alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu wa aina
yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na jimbo la Kalenga kwa jumla.
No comments:
Post a Comment