ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 6, 2014

USAHIHISHAJI WA MITIHANI SHULE ZA MSINGI KWA KUTUMIA KOMPYUTA WAPATA MAFANIKIO JIJINI DAR


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbado akifunga mafunzo ya siku 3 ya matumizi ya Fomu za OMR kwa walimu wakuu 254 wa shule za Msingi za mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Shaaban Robert.
Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda akitoa ufafanuzi kwa walimu wakuu wa shule za Msingi za mkoa wa Dar es Salaam kuhusu namna mkoa ulivyojipanga kutatua changamoto za elimu. 
Baadhi ya Walimu wakuu wa shule za Msingi jijini Dar es salaam wakifuatilia michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu maboresho ya matumizi ya mfumo wa OMR.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Matumizi   ya mfumo mpya wa  kufanya  mitihani kwa kutumia karatasi maalum  za OMR (Optical Mark Reader) na usahihishaji wa mitihani hiyo kwa njia ya kompyuta umeonyesha mafanikio  jjini Dar es salaam mara baada ya vitendo vya udanganyifu na wizi wa mitihani ya shule ya msingi kudhibitiwa.

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbado ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya siku 3 ya matumizi ya Fomu za OMR  kwa walimu wakuu 254 wa shule za Msingi za mkoa wa Dar es salaam.

No comments: