Mvua zaleta maafa Dar es Salaam.
Mvua
zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam, zimesababisha maafa
kutokana na baadhi ya magari kupinduka barabarani mengine kukwama kwenye
mashimo na msongamano wa muda mrefu kutokana na magari kuteleza na
miundombinu ya barabara kuharibika.
Akizungumza katika eneo la tukio Kongowe Mzinga
jijini Dar es Salaam kondakta wa lori lililopinduka katika barabara hiyo
Casmir Michael amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya mwenye
daladala kusimama ghafla mbele ya lori lao ndipo breki za gari lao
kukataa na tairi kupoteza mwelekeo kisha gari kupinduka.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali ya haisi wamesema
chanzo ni baada ya haisi kuigonga gari nyeupe iliyokuwa imeharibika
barabarani lenye namba za usjaili T591 CGP na kushindwa kushika breki
saa chache kabla halijatumbukia mtaroni kwa kuwa mbele kulikuwa na shimo
kubwa lililochimbika baada ya kunyesha kwa mvua.
Nao madereva waliokumbwa na adha ya mrundikano wa
foleni barabani wameiomba serikali kutengeneza makarabati imara na
barabara za pembeni ili magari yaweze kupita kwa urahisi zinapotokea
ajali kwenye barabara hiyo.
ITV imeshuhudia gari la magereza nalo likiwa
limenasa kwenye barabara ya pembeni hali iliyowalazimu askari magereza
kushuka kwenye gari lao kisha kulisukuma walipokwama wakiwa njiani
kuelekea wilayani Mkuranga mkoani Pwani kusindikiza mahabusu wao.
No comments:
Post a Comment