ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 6, 2014

VURUGU ZA WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA ZAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA



 Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo mchana baada ya Bunge hilo kuahirishwa ghafla kwa muda kutokana na kufuatia kutokea Sintofahamu baina ya wabunge waliokuwa wakirushiana maneno bila kujali utaratibu na kutishia kushikana mashati jambo lililomfanya mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Ameir Pandu Kificho kutangaza kuliahirisha kwa muda.
Na Augusta Mafoto, Dodoma
Katika hali ya isiyokuwa ya kawaida ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mchana kumeibuka mtafaruku baina ya wabunge na kuzua vurugu Kutokana na Vuruguru Kutokana na Hali ya Kutokuelewana kati ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mhe. Ole Sendeka, Kutoleana maneno na Mbunge Mwenzake wakati Mbunge Huyo alipohoji kuhusu Kanuni za kuendesha kikao hicho.
Habari na picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto





1 comment:

Anicetus said...

Huu ni mwanzo tu: Mhe Bakari alisema" mimi nilizungumza vizuri kuweka utaratibu mzuri na kupokea majedwali haya. Mheshimiwa mwenyekiti kwa bahati mbaya MDOGO wangu Ole Sendeka anadai kanuni ANAZIJUA VIZURI....lakini ninachosema sifikiri....sifikiri kama UNA UZOEFU WA KUJUA YA KUNISHINDA MIMI. " Mheshimiwa Mweneyekiti, toka mwaka 1980 nipo katika mabunge haya! Kwa hivyo sifikirii kama mtu kutoka SIMANJIRO miaka 10 iliyopita anaweza akaja hapa akasema kanuni za KUNIZIDI. Mimi sitaki niombe radhi.Ila ninachotaka kumfahamisha ni kwamba kuna watu wenye UJUZI zaidi kuliko yeye!!!. Hivyo awe na makini katika mazungunzo yake--."alisema Bakari kauli hiyo ilizidiasha mgawanyiko katika bunge hilo ambayo wajumbe walisimama na kuanza kupiga meza, na wengine wakizomea. Baadhi ya wajumbe walionekana wakirushiana maneno na hat kutaka kurushiana makonde:

Wabunge maalum- maisha yanaendelea, mungu ibariki Tanzania na watu wake.

source:issamichuzi.blogspot.com 3-5-2014