JESHI
la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha
Songambele wilayani Maswa mkoani hapa, kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto
wake kwa kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba ili aliwe na fisi.
Kamanda
wa polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo alisema ofisini kwake mjini
hapa jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane za usiku
wakati mtuhumiwa Baya Seni (30) akiwa amelala na familia yake kijijini
hapo, ndipo alipokurupuka ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na
kisha kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba.
Alisema,
Seni katika maelezo yake kituo cha polisi alisema alifikia uamuzi huo
kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani
uzoefu umeonesha kuwa watoto wa kiume wakikua hudai kupata mirathi
kutoka kwa wazazi wao .
Alisema
kinyume chake watoto wa jinsia ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa
mifugo atakapolipwa mahari ili waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigo
tena kwenye familia yake bali mzigo huo huhamia kwenye familia
atakayoolewa. Mtoto huyo aliokolewa na majirani baada ya kusikia kilio.
Mama
wa mtoto huyo Elizabeth Paulo alisema, mume wake alikuwa akimtesa sana
mtoto wake akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na kwamba hana
faida kwake.
1 comment:
Mambo ya Kitanganyika Tanganyika. Kaeni na balaa zenu huko huko. Musituletee ujambazi Zanzibar.
Post a Comment