Mike Lukindo enzi ya uhai wake.
Watanzania wa Wisconsin wanapenda kutoa shukurani kwa wote waliojaribu kuokoa kutokuchomwa moto kwa ndugu yetu, mpendwa wetu Mike Lukindo na pamoja na jitihada zote zilizofanyika tunasikitika kuwataarifu kwamba mpendwa wetu ilibidi achomwe moto na jana Ijumaa April 4, 2014 majivu yake walikabidhiwa familia yake kwa mtoto wa kwanza wa marehemu kwenda kuchukua majivu hayo. Mpaka mazishi yafanyike zilikua zinahitajika $6,000 pamoja na michango ya sisi tuliopo Madison, Wisconsin haikuweza kufikia idadi iliyokua inahitajika.
Watanzania wa Wisconsin wanawashukuru vyombo vya habari ndani na nje ya Marekani vilivyosaidia kusambaza habari ya ndugu yetu, mpendwa mwenzetu na Mtanzania mwenzte mpaka habari kuwafikia ndugu zake Tanzania.
Shukurani za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani hususani Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa mchango waliotoa na mara kwa mara Balozi kupiga simu kufuatilia maendelea ya msiba.
Sisi Watanzania wa Wisconsin kwa niaba ya familia tunasema asante na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atawazidishia, Asanteni.

6 comments:
Poleni Sana watanzania wenzangu . Sasa inabidi tufanye jitihada kila mtanzania aliyekuwepo ulaya achukue insurance (Westside) nssf. Hi insurance Inasaidia kisafirisha marehemu mpaka nyumbani Tanzania. its very affordable please tujaribu or even just read about it
http://www.nssf.or.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=240&Itemid=215
Mimi si advertise but passing the information maana I have witness how it works and say its very easy and simple.
May lord rest our friend in peace also poleni sana wanafamilia
NAKUUNGA MKONO MDAU HAPO JUU, KILA MGHAIBUNI AJIUNGE NA WESTADI. VIONGOZI WA JUMUIYA ZOTE WAHIMIZENI WATU KUJIUNGA NA BIMA HII.
KAMA MNAVYOTOKA MAJASHO KWA AJILI YA URAIA PACHA BASI TOENI JASHO ILI KUWAFIKIA WAGHAIBU WOTE HASA HAPA USA. AIDHA NAWAPA WAGHAIBU WA DMV KWANI HAWAJAWAHI SHINDWA KABISAA. IKIWA NI KUSAFIRISHA AMA KUZIKA HAWA JAMAA HAWAJAMBO SANA. NA WENGINE IGENI UMOJA WA DMV, HONGERA BRO. SANDALI AND YOUR CREW.
WABONGO WOTE TUACHE TABIA YA KUSAHAU KWETU. USIJIVUNIE HUO UHAI AMBAO NI WA KITAMBO KIDOGO SANA. ZAA WATOTO WAPELEKE KWENU NA KUWAONYESHA HATA MAKABURI YA BABU NA BABA ZKO ILI UKIFA WAKUPELEKE HUKO NA KUKUZIKA. KAMA UNAOA KE YEYOTE HAKIKISHA UNAMPELEKA KULE MADONGO KUINAMA AU UZUNGUNI AMA UHINDINI ILI KAMA SHIDA YOTOKEA WAJUE WAWASILIANE NA NANI?
MWISHO TUWE NA MAWASILIANO NA CONTACTS INFO ZETU ZIWE UPDATED KUANZIA BALOZI ZETU HADI KWA NDG ZETU KULE KWA MKONO,SHELUKINDO,MBWEWE,MOMBO,VUNJO,MASAMA,UYOLE,KWA MCHAMBA WIMA,MNAZI MMOJA,TOSAMAGANGA,KITETE NK
nataka kuliza hivi mmeshindikana kupelekwa kuzikwa kwa ndugu yetu mtanzania marehemu lukindo?imekuwaje mpaka amachomwa moto? ndo alivyoandika will yake hiyo au ndo 6000 hizo dollar zimeshindikana
naomba anayejua zaidi anijuvye tafadhali
NDG ZETU WOTE WA HUKO HAWAKUWA NA $6000. HABARI NDIYO HIYO YA MUJINI WISCO. WADAU ELEWENI JAMBO MOJA KWAMBA KAMA MAREHEMU ALITOA WILL YA KUCHOMWA TUSINGEANZISHA MICHANGO NA KUDODA KIASI HICHO. AIIIIBU KWETU SOTE NA JUMUIYA ZETU.
poleni sana watanzania wote kwa msiaba huu nimesikia kwamba si kwamba hawakuwa na hela hizo ile wengi wao wanamsema kama mtu haendi kwenye masiko ya wenzake hajihusishi na watanzania wenzake litakalo mpata hawamchangi wala kumsaidia.
inasikitisha sana kama tuko hivi jamani inasikitisha sana.
na jambo la pili wengi hawana imani na nssf wanasema ni ibinu za kisiana na wengi wanasiasa ndo wanakopa na hatochukua muda mrefu nssf itakufa tu ni bora uwe na life insurance yako ya kimarekani fununu hizi za mitaani nimezisikia so sijui ni kweli au vipi
poleni sana watanzania wote
Acha hizo asiyejishughulisha na wenzake katika jamii pia wenzake hawajishughulishi. Yeye hakutaka karaha za wabongo alipokuwa hai kwa nini wabongo wapende karaha zake?
Siku hizi vyama vya wabongo kibao kila state, kuna vya kidini, ukabila pombe, mpira, umbeya, nk. Yeye marehemu alichaguwa kutupwa kama mnyama ana bahati kachomwa!!! Asiye na masikie na asisikie!!!
You consume what you pick!
Dont judge me but ukweli ndo huo!!!
Kila la heri wasio kata bima, wala kuweka akiba, wala kuwa na familia tajiri, wala kuwa social au kuwa na marafiki wazuri!! msondo utaucheza mwenyewe!!!
Post a Comment