Kwa wakazi wa Moshi kuna barabara itokayo shirimatunda inapitia soweto soko la mitumba
Memoria, hii ni barabara hatarishi sana kwasababu magari makubwa yanayotokea upande wa chini kuja kuunga na barabara iendayo Arusha hayasimami kabisa wewe kama dereva unadiriki kufunga breki za gafla ukiuliza kwanini hivyo utasikia baadhi ya abiria wakitamka yakwamba magari makubwa hayana breki kwa hiyo ni halali yao kupita bila kusimama na kusubiri aliyeko kwenye highway apite kwanza, je hii ni kweli gari kubwa linakuwa halina uwezo wa kusubiri aliye kwenye highway apite kwanza? muda si mrefu kutakuja kutokea ajali mbaya sana kwenye hii barabara awa madereva wetu sijui kwanini wanakuwa wagumu wa kufuata sheria walizojifunza kwenye vyuo vya usafirishaji na hata kama hukujifunza na kupewa udereva tu kwa kununua driving licence endesha basi kwa kutumia akili ukiona hapa sasa hivi mimi sitakiwi kupita hapa natakiwa kupita pia huyo tajiri unayemwendeshea hilo gari lake kubwa la kubeba mizigo utakapopata shida nalo kwa kusababbisha ajali yeye atakuona tena kama wewe ulikuwa ni mfanyakazi wake anakuacha uangaike na kesi peke yako na kama gari lake limepona linatafutiwa dereva mwingine na kundelea na kumzalishia wewe unabaki na kesi yako mwenyewe madereva nawaomba muwe waangalifu sana hasa hii barabara ninayoingelea.
KILIO CHANGU NI HIKI TU KATIKA HIYO BARABARA ITOKAYO SHIRIMATUNDA KUPITIA SOKO LA MITUMBA HAPA MJINI MOSHI NI HATARISHI SANA TENA KUTOKANA NA HAYA MAGARI MAKUBWA SANASANA HAYA YANAYOBEBA SODA.
No comments:
Post a Comment