the QUARTZ Blog
Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari ya mtu mmoja
aliyekutwa amefia kaburini kwamba alikubwa na umauti wakati akifanya
jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya
matumizi ya mambo ya kishirikina.
Kwa mujibu wa Saturday Tribune la
Nigeria, tukio hilo limetokea
katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa
huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na
marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya
kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao
wakiwa salama.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na
kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hili
waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka
kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.
Saturday Tribune iliongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la
Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa
kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilikuwa chanzo cha kifo
chake. Na kwamba polisi hawajathibisha kuwa tukio hilo linatokana na
masuala ya kishirikina.
No comments:
Post a Comment