Friday, May 16, 2014

SULEIMAN TALL, DULA MBABE ULINGONI MAY 24

Bondia mzoefu wa ngumi za kulipwa nchini Suleiman said Galile ”tall” anategemea kupanda tena ulingoni may 24 katika ukumbi wa friends corner manzese kuzipiga na Abdalah Pazi “dula mbabe/kiroba” katika pambano lisilo la ubingwa. Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo katibu wa ngumi za kulipwa nchini na ndie anayesimamia mapambano yote ya utangulizi bw Ibrahim Abbas kamwe amesema, “galile na dula wamekubaliana kusheza siku hiyo ya jumamosi ya terehe 24 na watazipiga katika uzito wa kg76 wakiwasindikiza Karama nyilawila na Said mbelwa watakaogombania ubingwa wa UBO,hapo awali ilipangwa karama kuzipiga na Thomas Mashali ambae amepatwa na majeraha kutokana na ajali ya gari , pia siku hiyo kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi yenye ushindani , wakati Adam Ngange akimkabili Alan kamote wa Tanga, zumba kukwe atazipiga na kamanda wa makamanda, Ramadhan Kumbele ataoneshana umwamba na hasan kiwale “Moro best”, Bakari Dunda na Mbena Rajabu, huku madogo wanaokuja juu kwa kasi katika ngumi Idd Athuman atacheza na Julias Thomas kisarawe, Mwaite juma na Daud giligili. kamwe alimaliza kwa kusema mpaka sasa hakuna bondia mwenye matatizo wote wapo katika hali ya ushindani wanaisubiria kwa hamu hiyo siku ifikie wabanjuane kiukweliukweli na watu wategemee mashindano mazuri yenye uwezo mkubwa wa kusukuma masumbwi

No comments: