ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 9, 2014

KARDINALI PENGO AZINDUA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA MARIAN BAGAMOYO

Mwadhama Polykarp Kardinali Pengo ©Dar es Salaam Arch Diocese
"Hakuna taifa lililoendelea bila watu wake kupata elimu" Ni maneno ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo kikuu cha Marian, kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino.
Padri Valentino Bayo anasema kuwa wamefikia hatua hiyo kama hatua ya kuiunga mkono serikali katika kukuza masomo ya sayansi, maana taifa limepungukiwa kwenye sekta hiyo. Bayo ambaye ni meneja wa shule za Marian ambayo iko kuanzia shule ya msingi hadi sasa kuelekea elimu ya juu, amewataka watu kujikita kwenye elimu kwa kadri wawezavyo.
Mfuko wa hifadhi ya jamii wa ppf umehusika kwenye tukio hilo ambapo michango mingine imepatikana kwa njia ya wanafunzi na harambee iliyofanyika kwenye hafla hiyo jijini Bagamoyo, mkoani Pwani

No comments: