ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 9, 2014

WAZIRI MKUU ACHARUKA, AKATAA KUKAGUA JENGO LA ZAHANATI


ILE HALI ya kufanya kazi kwa mazoea (business as usual) iliyojengeka kwa baadhi ya watendaji wa
Serikali leo imewatokea puani watendaji wa Manispaa ya Dodoma wakati Waziri Mkuu alipoamua kufanya ziara kukagua miradi ya maendeleo.
Akiwa katika eneo la kwanza ambalo alipangiwa kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Mkonze asubuhi (Jumamosi, Juni 7, 2014) Waziri Mkuu alipokea taarifa ya ujenzi wa kituo na kubaini kuwa hawajafanya chochote ili kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa Machi 22, 2014.

No comments: