ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 22, 2014

RAIS KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA SONGEA-NAMTUMBO

Dkt.Jakaya Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation) Bwana Karl Fickensher wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi Kuzindua Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation) Bwana Karl Fickensher wakati wa uzinduzi wa Barabara ya lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na msaada kutoka kwa watu wa Marekani kupitia mfuko huo katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma. Picha na freddy Muro wa Ikulu

No comments: