Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Ajman Chamber Bw. Mohamed Al Janah (aliyepo kushoto mwa Mhe. Mjenga) na kufanya naye mazungumzo katika ofisi za Ajman Chamber, kwenye Falme ya Ajman.
Katika mazungumzo yao, wamegusia maeneo tofauti ikiwa ni masuala ya biashara kati ya Tanzania na Ajman, kuvutia viwanda vya Ajman kuwekeza Tanzania, masuala ya biashara na upatikanaji wa Ajira kwa Watanzania.
Kwa pamoja, wamekubaliana kuandaa ziara ya wafanyabiashara na viwanda vya uzalishaji kutoka Ajman kwenda Tanzania na kukutana na wenzao ili kutambua maeneo muhimu ya kuwekeza. Ziara inategemewa kufanyika kabla ys Novemba 2014.
Kuhusu ajira kwa Watanzania, Mhe. Mjenga amemuomba Mkurugenzi Mtendaji huyo, Bw. Mohamed Al Janah, kuangalia uwezakano wa kuanza kuajiri Watanzania wenye maarifa katika nyanja tofauti. Bw. Janah amemuhakikishia Mhe. Mjenga kuwa ataandaa mkutano mwingine na makampuni mawili waliyoingia nao mkataba wa kuajiri wafanyakazi wao, ili waangalie maeneo yanayohitaji wafanyakazi na kuanza kampeni za kuajiri kutoka Tanzania.
No comments:
Post a Comment