Siku moja baada ya Bunge Malumu la Katiba kufanya mabadiliko ya kanuni kwa ajili ya kuwabana wajumbe wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa Bunge hilo Samuel Sitta amepanga kumkabidhi Rais Jakaya Kikwete katiba mpya inayopendekezwa ifikapo Oktoba 31 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba,Yahaya Hamis Hamad, inaeleza kuwa kazi ya kupitisha ibara za katiba pamoja na kupiga kura itafanyika Oktoba 10 hadi 21.
“Kazi ya kupiga kura, kujadili na kupitisha masharti ya mpito itafanywa kwa muda wa siku tano na baadaye Oktoba 31 mwaka huu ndiyo siku ambayo Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba (Sitta) ataiwasilisha katiba hiyo inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa baada ya Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kukabidhiwa katiba hiyo na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Watanzania watataarifiwa siku maalumu ya kuipigia kura katiba hiyo kama wanaifiki au laa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katiba inayopendekezwa itatungwa ndani ya siku 82 ambapo bunge limeelezwa kuwa wajumbe watafanya kazi hiyo katika siku 60 za kazi ambapo kamati zote 12 zitaanza kuwasilisha taarifa zao ndani ya bunge hilo kunzia Septemba 2 hadi 8 mwaka huu.
Taarifa hiyo pia inaonyesha kwamba wajumbe wa kamati watajadili sura zote za rasimu ya katiba kwa siku 15 kuanzia Agosti 6 hadi 27 kabla ya kutoa fursa kwa kamati zote kuandaa taarifa za sura zote za rasimu ya katiba.
“Majadiliano ya taarifa za kamati ndani ya bunge maalumu yatafanyika kati ya Septemba 9 hadi 29 na baadaye Kamati ya Uandishi itaandika upya ibara zote za rasimu ya katiba kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba sita mwaka huu,” taarifa hiyo ilieleza.
Juzi, wakati Sitta akihutubia katika ufunguzi wa awamu ya pili ya Bunge hilo, alisema pamoja na maoni ya kila namna yanayoendelezwa na wanaharakati kujadili mchakato wa katiba nje ya bunge hilo, ni muhimu wahusika wakapunguza jazba, chuki na upotoshaji.
Kuhusu uhalali wa kuendelea kwa shughuli za bunge hilo, alisema pamoja na uhalali wa kisheria waliopewa pia wanao uhalali wa kisiasa kutokana na sifa za uwakilishi wao walizonazo pamoja na maudhui yaliyomo kwenye rasimu hiyo.
THELUTHI MBILI
Ili kufanikisha mpango wa kukabidhi katiba iliyopendekezwa Oktoba 31, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba watatakiwa kuiunga mkono kwa idadi ya walau theluthi mbili ya wajumbe wote watokao Tanzania Bara na pia idadi kama hiyo kutoka Zanzibar ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012.
Kwa mujibu wa kifungu cha 26 (2), Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sheria Namba 8 ya Mwaka 2011, kinachoongelea Masharti kuhusu Bunge Maalumu, kinasema “Ili katiba iliyopendekezwa iweze kupitishwa katika Bunge Maalumu, inahitaji kuungwa mkono kwa wingi wa theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalum kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu kutoka Tanzania Zanzibar,”
Aidha kifungu cha 28 (1) kinasema “Baada ya kutunga Katiba inayopendekezwa, masharti yatokanayo na masharti ya mpito, Bunge Maalumu litavunjwa na mamlaka ya kutunga masharti ya katiba inayopendekezwa,masharti yatokanayo na masharti ya mpito yatakoma,”
Aidha kifungu cha 28 (2), “Kuvunjwa na kukoma kwa mamlaka ya Bunge Maalum hakutachukuliwa kuwa kunaondoa mamlaka ya Rais kuliitisha tena Bunge hilo kwa lengo la kuboresha masharti yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa,”
Hofu kutokana na kufikiwa kwa idadi hiyo wakati wa upigaji kura inatokana na kutokuwapo kwa wabunge kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), linaloundwa na wajumbe wengi wa Bunge Maalum la Katiba wanaotoka katika vyama vikuu vya upinzani nchini vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
Ukawa walisusia vikao vya Bunge Maalum la Katiba kutokana na madai yao ya kutaka bunge hilo liache kubadili mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba, ambayo yanataka kuwapo kwa muundo wa muungano wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na wananchi kupitia maoni yaliyokusanywa na tume hiyo.
Hata hivyo, wajumbe wengi wanaoiunga mkono CCM wanapinga mapendekezo ya rasimu hiyo katika sura ya kwanza na ya sita yanayotaka muundo wa muungano wa serikali tatu na badala yake, wanasisitiza kuwapo kwa muungano wa serikali mbili lakini uliofanyiwa maboresho makubwa.
CCM WAZUIWA KUJADILI UKAWA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana aliIkutana kwa dharura na wabunge wa chama chake mjini Dodoma kwa zaidi ya saa sita na kuwapa maagizo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwataka waache kuwajadili wenzao wa Ukawa waliosusia vikao na pia waisaidie serikali kuepukana na aibu ya kutofikiwa kwa akidi.
Chanzo kutoka ndani ya kikao hicho kimeeleza kuwa Kinana aliwataka wajumbe hao wa CCM kuhakikisha wanaisaidia serikali kuhusu kutimia kwa akidi badala ya kuruhusu hali hiyo itumike kuivuruga nchi kisiasa na kuharibu mkakati wa kutwaa madaraka katika uchaguzi mkuu mwakani.
Aidha, ilielezwa zaidi kuwa Kinana aliwataka wajumbe wanaoiunga mkono CCM wasibweteke kutokana na mabadiliko ya kanuni yaliyofanywa ndani ya bunge maalum juzi na kuacha kuhudhuria vikao, akiwaonya kuwa kufanya hivyo kunaweza kukwamisha mchakato wa kupata katiba mpya..
Baadhi ya wajumbe wa CCM waliohudhuria kikao hicho waliiambia NIPASHE kwa sharti la kutotajwa kuwa, pamoja na mambo mengine, Kinana aliwapongeza wajumbe kwa michango waliyoitoa wakati wa kubadili kanuni za bunge hilo.
ZITTO KABWE
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amejitokeza hadharani kuhusu msimamo wake na kuungana na hoja za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) za kutoshiriki katika Bunge Maalum la Katiba ili kubaliki Katiba isiyotokana na rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilikusanya maoni kutoka kwa wananchi.
Miungoni mwa hoja ambazo ameziunga mkono kutoka kwa Ukawa ni pamoja kutohudhuria vikao vya Bunge Maluum la Katiba ili kubariki katiba ambayo haitakuwa na faida kwa wananchi pamoja na hoja ya kuwapo kwa muundo wa serikali tatu zilizoboreshwa.
Zitto alisema hayo katika kipindi cha mahojiano maalumu kilichorushwa na kituo kimoja cha televisheni jana na kueleza kuwa, pamoja na kuunga mkono hoja za Ukawa, lakini yeye hayupo upande wowote katika makundi yanayovutana kuhusu katiba mpya.
“Kuunga mkono hoja sahihi za Ukawa siyo kwamba ndiyo nipo Ukawa, hapana... sipo huko na wala sijishughulishi nao. Pia hata sipo kwa kundi lingine la Tanzania Kwanza,“ alisema Zitto.
Hatua ya Zitto kutoa kauli hiyo ilitokana na maswali yaliyokuwa yakiulizwa na muendesha kipindi hicho ambacho miungoni mwa maswali aliuulizwa ni kuweka wazi kwanini hayupo bungeni.
Akijibu swali hilo alisema kuwa hawezi kwenda katika Bunge hilo la Katiba kwakuwa ni kupoteza muda na kodi za wananchi kwani katiba itakayotungwa haitakuwa na faida kwa wananchi.
“Siwezi kwenda kushiriki Bunge hilo Maalum kwakuwa sipo tayari kubariki katiba ya kundi kubwa la upande mmoja ambayo najua baada ya muda mfupi itahitajika tena mabadiliko kwani Watanzania wa sasa si wa jana,“ alisema Zitto.
Kuhusu kuunga mkono hoja ya Serikali tatu alisema yeye anahitaji kuwapo kwa serikali tatu zilizoboreshwa na kufafanua kuwa itakuwa na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano huku kila nchi yaani Tanganyika na Zanzibar zikiongozwa na Mawaziri wakuu watakaotokana na idadi kubwa ya Wabunge wa vyama vya siasa vitakavyoshinda.
“ Tuna mifano kama hiyo Uingereza, India na Ujerumani. Vyama vinavyochagua Waziri Mkuu ni vile vilivyoshinda Wabunge wengi katika uchaguzi mkuu, sasa kwanini na sisi tusiige mfumo huo wa wenzetu lakini tukawa na rais mmoja na siyo marais wawili?” alihoji Zitto.
HUMPHREY POLEPOLE
Watanzania wametakiwa kuendelea kumkumbusha Rais Jakaya Kikwete kusimamia ajenda ya Tanzania kupata Katiba Mpya baada ya miaka 50 ya Uhuru na si kufanyiwa marekebisho.
Hatua hii imetajwa kuwa ni fursa pekee kwa Watanzania katika kushiriki upatikanaji wa Katiba hiyo, kutokana na marekebisho ya mwaka 1977 na 1984 kufanyika bila ushiriki wao.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole wakati mjadala wa wazi kuhusu Mchakato wa Katiba ‘Tulikotoka, Tulipo na Tunakokwenda’ ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) pamoja na Mtandao wa Wanawake na Katiba.
Alisema kumekuwa na kundi la watu wachache ambao kwa maslahi binafsi na ya vyama vyao wana nia ya kuvuruga mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
“Ninashangaa baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanataka kutuziba midomo, kwa kusema mijadala, makongamano kuhusu Katiba Mpya nje ya Bunge isijadiliwe, wakumbuke hata rasimu hii ya Katiba wanaoijadili ilitokana na hatua ya nne za awali kuanzia Tume ya mabadiliko ya Katiba, Ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi, na sasa ni Bunge Maalum,” alisema Polepole.
Alisema wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakijadili zaidi sura ya kwanza na ya sita huku wakiacha kujadili sura zote ambazo hazijawekwa wazi na kuleta utata katika muundo wa Muungano ambao kwa rasimu hii upo katika sura ya kwanza, sita, nane, 10 na 11.
Mwanaharakati kutoka TGNP, Gemma Akilimali, akizungmza katika mjadala huo, alisema wanawake walio wengi walishindwa kushiriki katika mchakato wa awali wa kukusanya maoni kutokana na kuwa katika shughuli za uzalishaji na kusababisha kutokuwapo kwa maoni yao katika rasimu hiyo.
“Mimi nilipata bahati kwenda mkoani Iringa kukusanya maoni kwa wananchi nilikutana mama mmoja akijishughulisha na ushonaji, nilimuuliza kuwa anafahamu masuala ya katiba cha ajabu alijibu hafahamu lolote akaomba ufafanuzi toka kwangu ilimradi alikuwa akiishi makazi ya Jeshi la Polisi,” alisema Akilimali.
Pia alisema wajumbe waliopo Bungeni wasihodhi masuala muhimu ya wanawake na kusema wajumbe wanatakiwa kujadili haki za wanawake na kubainishwa katika Katiba Mpya ambazo ni umilikaji wa ardhi na rasilimali, elimu, maji, kuheshimiwa kwa utu mwanamke na afya ya uzazi.
Imeandaliwa na Godfrey Mushi na Jacqueline Massano (Dodoma), Ashton Balaigwa (Morogoro), Christina Mwakangale, Hussein Ndubikile Na Raphael Kibiriti (Dar).
-----

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment