IKIWA ni tofauti ya siku moja kufanana kwa tarehe ya janga la moto jana Septemba 12 msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pilia ambapo moto wa kwanza ulizuka Agosti 13 mwaka huu na kusababisha mtafaruku kwa waumini wake pamoja na waislamu wengine kwa ujumla.
Msikiti huo ambao kwa mara ya kwanza uliuungua katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa ukarabati.
Ghafla jana ulizuka moto ambao unasadikika ulianza saa sita na nusu mchana jana katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha nne wa kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya kukabiliana na mtiwao wa taifa utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la msikiti huo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura alisema hadi wanafika eneo la tukio chanzo bado hakijafahamika.
Aidha Wambura aliongeza kwa kusema kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni chumba cha wasichana na magodoro manne yameungua.
“Katika janga la moto uliounguza madarasa mwezi uliopita Jeshi la Polisi lilinda timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu hiyohiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya mawili” alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya kutajwa majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema kwamba “ sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati tukivuta muda was ala ya Ijumaa ndipo tuikasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume wakikimbia huku na kule kwa taharuki hivyo chanzo hasa cha moto sisi hatukijui.
Licha ya kuwa hili ni tukio la pili la moto kutokea kwenye msikiti wetu ndazi ya siku chache tu huenda ikawa labda ni mwezi tu tangu moto wa awali ulipotokea imani yetu ya dini ya kiislamu inatukataza dhana hivyo wala hatumdhanii mtu yeyote kusababisha moto huu.
“Mwenyeezi mungu ndiye anaejua kila kitu hivyo tuna imani kubwa kwamba iko siku atafichua ukweli wa chanzo ama sababu za moto huu ila jambo la kushukuru ni kwamba moto huu umetokea muda ambao kila mtu ananguvu za kuuzima hilo ni jambo la kushukuru kwani laiti kama ungetoea nyakati za usiku hali ingekuwa mbaya” walisema kina mama hao.
Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida.Agosti 13 mwaka huu msikiti wa Mtambani uliungua moto .
Wananchi wakiwa nje ya Msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni wakishuhudia tukio la kuungua moto kwa mara ya pili msikiti huo Dar es Salaam jana.
Waumini wa msikiti huo pamoja na wananchi wakisaidia kuvuta mpira wa maji kwa ajili ya kuzima moto huo.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi eneo la tukio.
Askari wa Kikosi cha Uokoaji wakifunga mpira wa maji baada ya kuudhibiti moto huo.
Wananchi wakiangalia madawati na vyombo vingine vilivyookolewa katika tukio hilo.
Heka heka za uzimaji moto zikiendelea. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Waokoaji wakiwa wamebeba zuria wakiingiza ndani ya msikiti huo baada ya kuzimwa moto.
Waokoaji wakiwa wamebeba zuria wakiingiza ndani ya msikiti huo baada ya kuzimwa moto.
Mmoja wa waumini wa msikiti huo akilia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
picha na Habari na matukio
No comments:
Post a Comment