ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 29, 2014

ASIA IDAROUS KHAMSIN ANAKULETEA RED CARPET NA USIKU WA KHANGA PARTY LEO JUMAMOSI

Spice Modern Taarab Nov 29

Khadja Kopa, Bilal Mashauzi kuwasha moto
Na Andrew Chale
USIKU maalum wa kuenzi vazi la Khanga na magwiji wa taarab nchini 'Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab' unatarajia kulindima usiku wa Novemba 29 ndani ya Ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B huku pia ukitarajia kusindikizwa na gwiji wa mipasho Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi.
Kwa mujibu wa Asia Idarous Khamsin, mmoja wa wandaaji wa usiku huo, alibainisha kuwa kwa ushirikiano wa Fabak Fashions na Safari Carnival wameandaa usiku huo maalum kuenzi vazi la Khanga.
"Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab ni maalum kuenzi vazi hili la khanga ambapo pia watu wote watakaofika watavaa vazi maalum la khanga. Hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P." alisema Asia Idarous Khamisin.

Aidha, alisema wadau watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi.
Aidha, alibainisha kuwa, usiku huo pia kutakuwa na zulia jekundu 'Red Carpet' ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maalufu watakao jitokeza usiku huo ambao pia Dj John Dilinga atasimamia muziki wa zaman
Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival.

No comments: