ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 29, 2014

MAUAJI YATOKEA KWENYE DUKA LA NORDSTROM CHICAGO, ILLINOIS CHINI MAREKANI.

Mtu mmoja amefuatilia risasi mwanamke mmoja aliyesemakana ni rafiki yake wa kike na baadae kujifyatulia risasi yeye mwenyewe siku ya Ijumaa ndani ya duka la Nordstrom kwenye mji wa Chicago jimbo la Illinois mida ya saa 2:30 usiku.

Mwananmke huyo alikua ni mfanyakazi kwenye duka hilo na alikimbizwa hospitali akiwa na hali yake ni mbaya baada ya kufyatulia risasi na mwanaume ambaye inasemekana alikua rafiki yake wa kiume ambye yeye alikufa papo hapo kwenye tukio.

Hakuna mtu mwingine ndani ya duka hilo aliyejeruhiwa na polisi bado hawajataja majina ya mwanamke aliyepigwa risasi na mwanaume aliejiuua wala umri wao kwa madai kwamba uchunguzi bado unaendelea.

Maduka mengi siku ya Ijumaa baada ya Thanksgiving hujaa watu sana kwani siku hii huitwa Black Friday ambayo maduka hufanya punguzo ya bei ya bidhaa zilizopo dukani.

No comments: