Mrembo na muigizaji wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa ya rohoni kwamba hatokaa amsamehe mzazi mwenziye, Malick Bandawe.
Akizungumzia swala la kurudiana na mzazi mwenzake, Ndauka alisema alishawahi kufuatwa na mzazi mwenzake huyo kwa lengo la kumuomba msamaha ili waendelee na mapenzi yao lakini hakuwa tayari kumsamehe.
“Kuachana tumeshaachana, kama kurudi huwa inatokea lakini kwangu sipo tayari tena kumsamehe, anaweza kutokea mtu mwingine wa kunipenda ingawa kwa sasa nahitaji kupumzika kwanza,” alisema Rose.
Rose na mzazi mwenzake waliachana mwaka jana huku wakificha sababu za kuachana kwao.
PICHA: Rose Ndauka akiwa na mzazi mwenziye, Malick Bandawe
GPL
No comments:
Post a Comment