ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 14, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI





Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameondoka nchini tarehe 13 Januari 2015 kwenda Urusi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mhe. Sergey Lavrov.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.


Mhe. Membe anatarajiwa kutumiafursa hiyo kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na Urusi, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na ubadilishanaji wa teknolojia. Tanzania inaweza kufaidika na utaalamu wa Urusi katika sekta za uzalishaji wa nishati, uvuvi, afya, kilimo na huduma. 



Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Tarehe 14 Januari, 2015.

No comments: