ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 26, 2015

CHID BENZ AACHIWA HURU BAADA YA KULIPA FAINI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.


CHIDI BENZ HURU:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya kulevya.-GPL

1 comment:

Anonymous said...

No wonder hii biashara haishi, kwa hizi hukumu ndogox2 itabidi watanzania tujiandae kisakologia kuweza kiishi na mateja.