ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 26, 2015

Mradi wa maji kuwakomboa wananchi 247,500 K’njaro


Profesa Jumanne Maghembe.

Mwanga. Serikali imeanza ujenzi wa mradi wa maji utakaowanufaisha wananchi 247,500 katika vijiji 28 vya wilaya za Mwanga na Same, mkoani Kilimanjaro.

Mradi huo utakaogharimu Sh142 bilioni, unafadhiliwa na Serikali na taasisi na mashirika ya misaada ya kimataifa kutoka nchi za Uarabuni.

Taasisi hizo ni pamoja na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo kwa nchi za Afrika (Badea), Mfuko wa Ofid unaojumuisha nchi zinazozalisha mafuta (Opec), Saud Fund for International Development na Mfuko wa Msaada wa Kuwait.

Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alisema jana kwamba mkandarasi ambaye ni Kampuni ya Karafi International ya Kuwait, ameanza ujenzi wa mradi huo.

Profesa Maghembe alisema awamu ya kwanza ya mradi huo utakuwa na sehemu tatu na kugharimu Sh142 bilioni.

Alisema kazi nyingine itakuwa ni kutoa maji Kisangara na kuyasukuma hadi Mlima Kivengere.

Alisema mradi huo utanufaisha pia vijiji vya Kiria, Mangulai, Njiapanda, Kiti cha Mungu, Nyabinda, Kagongo, Lang’ata Bora, Handeni na Tingat

Mwenyekiti wa Kamati ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Enea Mrutu alisema Rais Kikwete na Profesa Maghembe wameacha kumbukumbu ambayo haitasahaulika. MWANANCHI

No comments: