ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 18, 2015

Makamu wa Rais akagua mzani wa Kisasa wa Vigwaza na kufungua barabara ya Msoga – Msolwa km 10

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuhusu Mzani wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao umekamilika kwa asilimia 99.8.
Mzani wa Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akihutubia wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya kuukagua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani walioathirika na kimbunga kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba zaidi ya 40 katika kijiji hicho pekee.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akicheza ngoma pamoja na kikundi cha ngoma cha Msoga kusherehekea ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa yenye urefu wa km 10. Barabara hiyo itapunguza msongamano wa magari katika eneo la Chalinze.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na watumishi wa TANROADS mara baada ya kukagua Mzani wa Vigwaza.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu ambaye pia ni Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi wa Mzani wa Vigwaza.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakielekea kwenda kumpokea Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mzani wa Vigwaza mkoani Pwani. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi

No comments: