Mama amemuua mwanae baada ya kutaka kumuondolea aibu ya kuwa na masikio makubwa.
Inadaiwa mama huyo amesababisha kifo hicho akidhani kwamba mwanae akibaki na masikio makubwa yatamfanya akose raha maishani mwake kulingana na sheria za Uturuki atakabiliwa na kesi ya mauaji.
Nuray Sacan mwenye umri wa miaka 37 alitoa kiasi cha fedha ili mwanae aweze kufanyiwa upasuaji kwenye hospital ya Gazi jijini Ankara lakini oparesheni hiyo haikuweza kufanikiwa baada ya masikio hayo kubaki katika hali ile ile.
Mama amedai kuwa alimpeleka mwanae chooni muda wa asubuhi lakini alishangaa kumuona mwanae akiwa amejinyomga kwa kutumia nguo yake.
Nuray baada ya kuona mwanae amepoteza maisha alitaka kukimbia kwenye gari lake lakini alijikuta akikimbilia gari tofauti na la kwake.
Mama huyo alikiri kufanya mauaji hayo pale aliporudishwa hospitalini kwa gari la wagonjwa
Sacan aliwambia polisi kuwa”masikio yake yalibakia kuwa makubwa hata baada ya kufanyiwa upasuaji”
No comments:
Post a Comment