Mwenyekiti wa WAMA, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete
Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma Kikwete atakabidhi msaada wa mashine ya kupimia Kansa ya Matiti katika Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo tarehe Ijumaa Februari 27, 2015 saa tatu na nusu (3:30) Asubuhi.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Makao Makuu ya JWTZ, Ngome, Upanga jijini Dar es Salaam iliyotolewa leo Alhamisi Feb 26, 2015, imesema makabidhiano hayo yatafanyika kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba atapokea msaada huo wamashine kwa niaba ya Jeshi.
No comments:
Post a Comment