Miss Singida kanda ya kati 2014/15,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania.
Shule tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika kuwakomboa kielimu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu.
"Watoto wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani
Msaada huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu. Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.
Tafiti mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha yake ya baadae.
Kwa upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za msingi.
"Msingi wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris
Doris Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya kitamaduni.
No comments:
Post a Comment