ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 26, 2015

Wafuasi watatu wa IS,wakamatwa Marekani

Wapiganaji wa Islamic State
Maafisa wa Polisi nchini Marekani,wamewakamata wanaume watatu kwa njama za kuwaunga mkono wanamgambo wa dola ya kiislam Islamic State.

Wanaume wote hao ni wakaazi wa mji mkuu wa nchi hiyo New York. Wawili kati yao wanatokea Kazakhstan na Uzbekistan, na mwingine ni wa kutoka Uzbek yeye alimakatwa mjini Florida.

Wawili kati ya wanaume hao walikuwa na mpango wa kusafiri kuelekea nchini Syria

Kwa mujibu wa Shirika la Ujasusi la Marekani FBI watuhumiwa wawili kati yao walitishia kuwaua maafisa wa polisi kama wasingeweza kusafiri kwenda Syria.

Hata hivyo mtuhumiwa mmoja kati ya watuhumiwa hao alikuwa na mpango wa kumuua rais Marekani Barack Obama,wamesema FBI.

Kamishina wa polisi mjini New York , William Bratton anasema maneno yao ndiyo yanayodhihirisha nia yao.Hata hivyo inadaiwa kuwa ni dhahiri kutokana na matamshi yao walikuwa na mpango wa kusafiri hadi nchini Syria, baada ya kukamilisha malengo yao ya kijipatia silaha ambazo wangezitumia kuwashambulia maofisa wa polisi.

Bratton amesema ilikuwa ni mpango wao wa wazi kwamba hawakuhitaji kwenda,huku malengo yao ikiwa ni kujipatia silaha kama vile bunduki aina ya mashine gani, kwa lengo la mashambulizi maalum dhidi ya maofisa wa polisi ambapo maneno yao ya kuhamasishana yalikuwa wazi kwa mjibu wa maneno yao.

Nje ya mahakama mjini New York walikofikishwa washitakiwa wawili mwanasheria wa washitakiwa hao, Adam Parumata ameelezea kutoridhirishwa na mwenendo wa mashitaka hayo dhidi ya wateja wake.

"Kama tuhuma hizi ni za kweli,na bado ni tuhuma tu, zinatufanya kujiuliza maswali mengi kwa jinsi serikali inavyowachukulia vijana hawa,na watu wa dini ya Kiislam ndani ya Marekani. Kwani wapo katika uangalizi mkali na wa aina yake,hakuna ruksa kujibu,kuzungumza, kudadisi wala kueleweshwa. Kinachofanyika ni mbio mbioni kuwafungulia mashtaka, kuwaweka kizuizini. Nataka kusisitiza jambo kwa kila mtu leo kuwa haki ya mshitakiwa ni kwamjibu wa sheria za Marekani,hivyo tunafanya kila linalowezekana kupigania haki katika kesi hii kwa lengo la kulinda haki”amesema Parumata.

BBC

No comments: