ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 26, 2015

Ebola:Mfanyakazi apoteza maisha

Mfanyakazi wa kituo cha yatima Augustine Baker

Raia mmoja wa Sierra Leone aliyekuwa akiwatunza Watoto walioachwa yatima kutokana na ugonjwa wa Ebola amekufa kutokana na ugonjwa huo.

Augustine Baker alifikishwa katika kituo cha matibabu baada ya kuugua juma lililopita.

Baker alikuwa akifanya kazi katika Kituo cha Watoto yatima kinachoendeshwa na kituo cha msaada kutoka Uingereza.Kituo hicho kiko nje ya mji wa Freetown.

Watoto 33 na Wafanyakazi saba katika nyumba ya yatima St George, wamewekwa katika Karantini tangu Bwana Baker alipobainika kuwa na Virusi vya Ebola.

Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2004 mpaka pale Ugonjwa wa Ebola ulipoingia, kituo kilijikita zaidi katika kuwaokoa Watoto wa mitaani.

Mwaka jana kituo kiliwasaidia Watoto takriban 200 walioachwa na familia kutokana na Ebola.

Ebola imeua zaidi ya Watu 9,500 nchini humo,Liberia na Guinea.

Lakini katika kipindi cha majuma ya hivi karibuni, kasi ya maambukizi ya Ugonjwa huu imepungua na Serikali za nchi tatu zimeahidi kumaliza kabisa tatizo hili ndani ya miezi miwili ijayo.

BBC

No comments: