Lowassa ambaye alirejelea kauli yake ya kwamba yeye si tajiri bali ni tajiri wa marafiki, alichangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya sare za shule kwa wanafunzi ambao nguo zao ziliteketea.
Aidha mwenyekiti mtendaji wa makampuni IPP, Reginald Mengi akichangia shilingi milioni 25 kwa ajili ya vitanda na Kampuni ya A to Z ikichangia ujenzi wa mabweni mawili yaliyo ungua moto hivi karibuni.
Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Anoji Shah (aliesimama) akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli umuhimu wa elimu na pia kutangaza msaada wa ujenzi wa mabweni yote mawili yaliyoteketezwa kwa moto wiki mbili zilizopita.
Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa akizungumza wakati alipotembelea shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli, mkoani Arusha jana. Mbunge huyo alichangia shilingi milioni 3 kwaajili ya sare za wanafunzi zilizoungua wakati wa ajali ya moto shuleni hapo. Kampuni ya Ato Z wameahidi kujenga mabweni mawili ya shule hiyo yaliyounga na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi aliyechangia shilingi Milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa vitanda.
No comments:
Post a Comment