ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 18, 2015

“WOMEN MAKE IT HAPPEN” - EVENT

Siku Ya Wanawake Dunia huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 8, mwezi wa tatu. Siku hii huadhimishwa kwa shughuli mbalimbali na kutambua mchango wa mwanamke katika maendeleo ya Jamii.

Mwaka huu kitaifa Siku hii itaadhimishwa mkoani Morogoro lakini kampuni ya TruMark ya mjini Dar es Salaam imeandaa warsha maalum katika maadhimisho hayo ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam Machi 7 mwaka huu.Kauli mbiu ya Siku hii ni Women Make It Happen’ ikiwa inamaanisha wanawake wanafanikisha.
TruMark imeamua kufanya tamasha hili, baada ya uzoefu tulioupata katika shughuli zetu za mafunzo ambazo tunatoa kwa watu mbalimbali, tulioana kuna changamoto mbalimbali ambazo wanawake wanazipata.


Hii likafanya tuone kuwa Siku Ya Wanawake ni jukwaa ambalo linaweza kukutanisha wanawake katika kada mbalimbali na kuzungumza mambo yao katika kujikwamua kiuchumi na kujifunza kwa wengine ambao walipitia changamoto hizo lakini leo hii wameweza kufika mbali baada ya kupambana.

TruMark imepata Baraka zote kutoka Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto katika kuandaa siku hii muhimu. Kwenye maadhimisho haya, kutakuwa na mada ambazo zitatolewa na wanawake kutoka katika kada tofauti, juu ya uongozi, biashara na uchumi, ujasiriamali.
Lakini pamoja na elimu ambayo itatolewa kutakuwepo na burudani pia kutoka kwa wasanii wanawake maarufu na chipukizi nchini ambao wataungana na wanawake wengine kusheherekea siku yao hii.

Wanawake wanakaribishwa kushiriki katika siku hii ili kuweza kupata elimu ambayo itawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku. Kwa upande mwingine tunatoa wito kwa wadhamini kujitokeza ili kufanikisha siku hii kwani mama ndiye kiungo cha familia.

Na kama ijulikanavyo kuwa katika kila mwanaume mwenye mafaniko basi nyuma yake yuko mwanamke shupavu.

Trumark tunawakaribisha wadau na wahisani kutoa ufadhili. Mchango wowote utatambulika katika kufanikisha tamasha la wanawake litakalowawezesha walengwa ambao ni wanawake kufikia malengo yao kwa kutumia changamoto na kuzibadili kuwa fursa.

Asilimia 10 ya mapato yatakayopatikana kwenye tamasha hili yatakwenda kusaidia wasichana kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi. Wasichana hawa watatokana na shule tutakayoichagua.

Kuhusu TruMark hii ni kampuni inayojihusisha na utoaji mafunzo mbalimbali ya uongozi, biashara na ujasiriamali yenye lengo ya kuboresha ufanisi kwa matabaka mbalimbali katika jamii.
MWISHO.
Agnes Mgongo
Managing Director
TruMark
Human Potential Skills Development
Josam House Complex -Mikocheni
P.Box 12382- Dar es Salaam
Mobile: +255 754 095 017 / 658 095017
Email: amgongo@trumark.co.tz
Website: www.trumark.co.tz

No comments: