Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na ujumbe wa shirikala fedha la kimataifa (hawapo kwenye picha ). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa IMF kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh akiwa na ujumbe kutoka IMF wakizungumza na ujumbe kutoka Tanzania (hawapo kwenye picha).Katika kikao hicho walizungumzia zaidi suala la Tanzania kuzidisha nguvu katika kuboresha sera za kukuza uchumi.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akifurahia jambo aliloambiwa na Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki wakati wa mkutano uliofanyika kati ya ujumbe kutoka Tanzania na Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akitoa maelezo ya jinsi Tanzania inavyoboresha uchumi wake kwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa (IMF)kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh wa katikati. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba
Bw. Kamran Khan Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni za mfuko wa Changamoto za Milenia akizungumza katika mkutano wa (MCC/Chamber of commerce )akisikilizwa kwa makini na wa jumbe kutoka mfuko wa Changamoto za millennia na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya aliyekaa mbele.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya, akifuatilia kwa makini mkutano huo wa mfuko wa Changamoto za millenia/Chamber of Commerce Uliokuwa ukifanyika hapa mjini Washington DC.)
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akizungumza katika mkutano huo wa Changamoto za Milenia/Chamber of Commerce uliofanyika mjini Washington DC. Aliyeko nyuma ya Mhe Waziri ni Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili
No comments:
Post a Comment