ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 8, 2015

MREMBO MBONGO AFIA CHINA!

Mwanadada Rehema Mohamed anayedaiwa kufia China.

Imelda Mtema
Mrembo Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Rehema Mohamed (30), anadaiwa kufia katika Mji wa Shanghai nchini China wiki mbili zilizopita baada ya kuugua kwa muda mrefu hadi mauti yalipomfika huku ndugu zake wakichanganyikiwa kutokana na taarifa za kifo hicho.

Habari zaidi kutoka kwa aliyekuwa rafiki wa karibu wa Rehema nchini China, (jina lake linahifadhiwa) zinasema kuwa wamekuwa wakihangaika ili kupata fedha za kusafirisha mwili huo lakini imekuwa ngumu kupatikana.
Chanzo hicho kilisema kuwa kimefanya mawasiliano na baadhi ya ndugu wa marehemu ambao nao wanajikusanya kwa ajili ya kupata fedha hizo ili kuurudisha mwili nyumbani Dar kwa mazishi.

“Yaani huku tunapata tabu sana na tuna uchungu kwa kuwa fedha zilikuwa zikihitajika nyingi sana lakini tunashukuru taratibu zinaenda sawa karibu tutaleta mwili nyumbani,” alisema rafiki huyo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kuwa kifo cha ndugu yao ni pigo kubwa ukizingatia amefia ughaibuni na fedha za kumleta zinahitajika nyingi hivyo wamekaa na kumuomba Mungu ili mwili ufike Bongo waupumzishe.

“Msiba wa mdogo wetu umetupa wakati mgumu sana jamani, ukizingatia amefia mbali sana na kumleta huku ni fedha nyingi mno, hivyo tunamuomba Mungu tu ili mwili ufike na tuupumzishe katika makaburi ya nyumbani,” alisema ndugu huyo.

GPL

No comments: