Mkutano wa Raraza la pili la Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu likiendelea.
Mwenyekiti
wa Baraza la pili la
Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Ndugu,Jairo
akifafanua kazi za Baraza hilo katika Vyuo vya uhasibu Nchini.Naibu
Waziri wa Fedha(S) Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na wajumbe wa Baraza
hilo,Kubwa amesisitiza mfumo mpya wa uajiri wa watumishi wa Umma ambao
utakidhi mahitaji ya wahadhiri vyuoni na hata kwenye Taasisi
zingine,Taasisi za Elimu na fedha zingepewa mamlaka ya kuajiri kutokana
na uhitaji wao mara baada ya fungu la bajeti la kuajiri kupita,Hii
itarahizisha ukiritimba wa kazi kwa mazoea na taasisi hizi kukosa
watumishi wa kutosha kuhudumia idadi ya wanafunzi/wahitaji huduma.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza hilo wakisikiliza hotuba ya Mh:Mwigulu Nchemba
ambaye amewahakikishia kuwa Wizara ya fedha itaendelea kutoa na kuwekeza
nguvu zake kwenye Taasisi za elimu hasa uhasibu kwaajili ya kuhakikisha
vyuo vinatoa huduma stahiki.Prof.Kamzora Makamu wa Chuo kikuu cha Mzumbe
akitoa shukrani kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwakuonesha njia kuwa Vijana
wanaweza kufuta Utumishi wa Mazoea,tena katika swala la ajira.Profesa
amesema Mwigulu anajibu wazi wazi mambo yote ambayo Mwl.Nyerere
aliandika kwe ye Kitabu chake cha TUJISAHIHISHE"Sijawahi kusikia
kiongozi nchi hii anaweza kuwa na maono kama yako tena ya
kimabadiliko,Tumia maono haya kuifikisha Tanzania kwenye neema ambayo
wengi wanapenda kuifikia"alisema Prof.Mh:Naibu
waziri wa Fedha akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi /wajumbe wa
Baraza la pili la Watumishi wa Taasisi za Uhasibu ambao hii leo Baraza
lao limefunguliwa Rasmi na Mh:Mwigulu Nchemba.
Picha/Maelezo na Festo Sanga-Bagamoyo
No comments:
Post a Comment