Texas Black Belts club Seminar , imeandaliwa na Sensei Ramon Veras, Dan 7, Okinawa Goju Ryu Kyokai, mjini Houston, Texas tarehe 19 April, 2015. Pia ni sehemu moja ya maandalizi na marekebisho ya mbinu na ufundi wa vipande tofauti katika mfumo mzima wa Sanaa na tayari kwa baadhi ya washiriki kwa msafara wa kwenda kwenye chimbuko la Karate huko Okinawa, Japan. Sensei Rumadha Fundi, ni mmoja ya wawakilishi wa Goju Ryu Jundokan, atayoiwakilisha Tanzania kwenye msafara huo..
Baada ya takriban miaka 23 sasa, sensei Rumadha Fundi “Romi”, anarejea tena chini Japan kama alivyofanya mwezi May mwaka 1992. Safari hiyo ya mwezi June kwenda Naha City, Okinawa kwa njia ya Los Angeles, Tokyo na hatimaye Naha City, Okinawa. Sensei Rumadha amepewa mwaliko kama mwakilishi wa Jundokan Tanzania, kwa niaba ya kuwa mteule na mwakilishi wa chama hicho cha mtindo wa Okinawa Goju Ryu, chini ya rais wake ambaye ni mtoto wa Eiichi Miyazato mwanzilishi wa chama hicho Sensei Yoshihiro Miyazato “Kancho”, na hatimae kupewa jukumu la kusambaza Jundokan nchini kote akiwa“Tanzania Chief Instructor ” na kupewa madaraka ya kutowa idhini na mikanda ya wawakilishi wa Jundokan nchini Tanzania na utambulisho wa kutowa vyeti ( Dan Certificate) kutoka, Naha, Okinawa. Sensei Rumadha anashikilia Dan 6 toka Tanzania Karate-do Federation, na Dan 3 toka Jundokan Kyokai.Lengo na madhumuni ya sensei Rumadha ni kusambaza ufanisi wa Goju Ryu na mbinu za “Muchimi” ni undani halisi wa utumiaji mbinu kifasaha na kitamaduni kama ifanyavyo huko Okinawa, Japan. Sensei Rumadha, atafanya mazoezi katika dojo ambayo mwalimu wake yeye Sensei Bomani na Master Morio Higaonna walikuwa wanafunzi hapo miaka 45-50 iliyopita. Pia Sensei Rumadha, atatembelea sehemu zenye historia ya mwanzao wa Karate na makaburi ya waanzilishi wa Sanaa na makumbusho ya Karate na vitongoji vyake kama, Naha, Shuri na Tomari, Okinawa , Japan.
Nia na madhumuni makubwa ni kutaka kuiendeleza Goju Ryu Karate Tanzania na hatimae kuwa na walimu wenye utambulisho huko, Okinawa, Japan na kuleta maendeleo na maslahi ya kimaisha kama mwalimu wa Karate. Pia Sensei Rumadha alisema “ Tapenda kubadilisha mfumo wa jinsi Goju Ryu inafundishwa Tanzania. Tawapa mwaliko wanafunzi wote wenye nia ya mafanikio na utambulisho toka Okinawa, kuwa chini ya uongozi wangu na kuendeleza utamaduni wa Goju Ryu. Goju Ryu ina matawi mengi na uongozi tofauti, mimi napendelea kuwa na shina la Okinawa Goju Ryu Karate – do, lililowekwa na waanzilishi wa mtindo huo; lengo ni kuwa na Goju Ryu halisi na sio mabadiliko”, alisema Sensei Rumaha..
CHOJUN MIYAGI ( Goju Ryu Karate )
Mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Master Chojun Miyagi , mzaliwa wa Higashimachi, Naha, Okinawa April 25, 1888. Miyagi alianza mafunzo ya karate akiwa na umri wa miaka tisa (9), chini ya Ryuko Aragaki, ambaye alimtambulisha kwa Kanryo Higashionna (Higaonna Kanryo) wakati alipofikisha umri wa miaka 14.
Mafunzoni China.
Mwezi May 1915, kabla ya kifo cha Kanryo Higashionna, Chojun Miyagi alikwenda jimbo la Fujian, huko China. Alipokuwa China, Miyagi aliweza kutembelea kaburi la mwalimu aliyemfundisha mwalimu wake Karyo Higashionna aitwae RyuRyu Ko. Baada ya kifo cha mwalimu wake Karyo Higashionna, October, 1955, Miyagi alifanya safari yake ya pili China, huko Foochow. Pia inaaminika kwamba, muda aliyokuwa huko China, Master Miyagi, alijifunza Shaolin na Pakua Chuan huko Fuzhou Shaolin Temple. Hapo ndipo kwa mara ya kwanza, master Miyagi alipopata kuona mbinu za mikono mitupu ( Rokkishu) yenye msisitizo wa kinga za duara ya kiganja na ngumi zenye mfano wa Kata, na muonekano wa kijihami nakinga na mashambulizi. Hapo ndipo alipotunga “Tensho kata”toka katika misingi ya Sanaa ya Shaolin.
Kutoka katika mchanganiyiko wa mtindo wa Naha –te (Mkono wa Naha), akaanzaisha mtindo mpya kabisa. Japo ya kuwa ni mtindo mpya bila ya jina, alichukua muda hadi mwaka 1929 ambapo Miyagi akaipa jina Sanaa ya mtindo wake “Goju-Ryu” akimaanisha “Ngumu na Laini”.
Kurudi Japan
Baada ya miaka mingi huko Chini, Miyagi alirudi mjini Naha na kufungua shule au dojo.Alifundisha kwa miaka mingi na kuwa maarufu katika kisiwa cha Okinawa, na hata bara, Japan. Mtindo wa Goju Ryu, ni mtindo wa kwanza kutambulika na shirikisho la Sanaa za kujihami la Japan, “Dai Nippon Butokukai ”. Alitambulisha Karate katika jeshi la polisi wa Okinawa, shule za sekondari na jamii zote. Akatunga kata ya Sanchin, ambayo ina maana ya hali ngumu ya tafsiri ya Goju Ryu, pia akatunga Tensho kata kama upande wa laini wa Goju Ryu Karate. Hizi kata zina maadilifu ya jinsi na namna Miyagi alikuwa na nia kufundisha mtindo wa ngumu na laini. Na moja ya hizo change moto ni mfano wa kata ya juu na mwisho za Goju Ryu, inayoitwa “ Suparinpei “ inaundani wote wa tabia na mwenendo wa Goju Ryu. Pia Miyagi, alikuwa anaipenda sana kata iitwayo “ Shisochin “. Kata ya Tensho, inamaadili mengi toka kwa ndege aitwae “ White Crane kata ,”Ryokushu ”. Pia Miyagi alitunga kata za msingi kama vile, “ Gekisai Dai Ichi, Gekisai Dai Ni ” mwaka 1940. Alitumia mbinu nyingi toka katika kata ya Suparinpei na kuongeza kata zingine kama vile, “ Sanchin &Saifa “ambazo ni za ngazi ya juu pia.
Baada ya kifo chake Octoba, mwaka 1953, wanafunzi wa ngazi ya juu wa Master Miyagi kwa wakati huo ni; Seko Higa, Eiichi Miyazato (Mwanzilishi wa Jundokan dojo), Meitoku Yagi ( mwanzilishi wa Meibukan Dojo) ambae alipokea sare au uniform na mkanda wa Master Miyagi toka katika familia ya Miyagi, Seikichi Toguchi (mwanzilishi wa Shorei - Kan Goju Ryu), na kwa upande wa bara ya Japan Gogen Yamaguchi (mwanzilishi wa International Karate-do Goju Kai) baada ya
kujifunza kwa Miyagi, aliteuliwa kama mwakilishi wa Goju Ryu bara la Japan mbali na visiwa vya Okinawa.
EIICHI MIYAZATO ( mwanzilishi wa Jundokan dojo)
Master Eiichi Miyazato, alijiunga na Ryukyu ( Okinawa) polisi kwa ushauri wa Master Miyagi mwaka 1946. Alikuwa anafundisha chuo cha polisi kama msaidizi wa Master Miyagi ambaye alikuwa anafundisha jeshi la polisi la Okinawa. Eiichi Miyazato, alikuwa anafundisha Judo pia. Baada ya kifo cha Master Miyagi 1953, Miyazato, alirithi vifaa na vitu vyote alivyo wacha Master Miyagi, hata uniform (Gi) na mkanda (obi) toka kwa familia ya Miyagi. Hapo ndipo alipo anza kufundisha dojo iliyowachwa na master Miyagi itwayo “ Garden Dojo “
Tarehe 20 mwezi March, 1988, Okinawa Goju –Ryu Karate- do Kyokai, ilimuenzi na Dan ya 10 ya Karate na pia kupewa Dan ya 7 ya Judo toka “Kodokan”, na kuwa rais wa
Okinawa Judo Federation “ wakati huo.
Master Eiichi Miyazato alifariki mwezi wa disemba, mwaka 1999, Naha , Okinawa. Juu ya kifo chake, Kodokan ilimuenzi na Dan ya 8 ya Judo. Wengi wa wanafunzi wa Eiichi Miyazato ni pamoja na ;
Chuck Merriman, Nanko Minei, Keikichi Nakasone, Kenei Shiabuku, Masaji Taira, Koei
Teruya, Ronald Yamanaka, Tony Foster and Tetsunosuke Yasuda. Miyazato's dojo is now run by his son, Yoshihiro Miyazato.
Riyosei Arakai, Shinzo Chinen, Teruo Chinen, Yoshio Hichiya, Morio Higaonna, Koshin Ihan, Shinichi Iribe, Masanari Kikukawa, Seikichi Kinjo, Tetsui Gima, Tsuneo Kinjo, Atsumi Lida, Kenei Shimabukuro, Hiroshi Ganaha, Kazuya Higa, Hisao Sunahawa, Richard Barrett, Mike Clarke, Chuck Merriman, Nanko Minei, Kekiichi Nakasone, Kenei Shiabuku, Masaji Taira, Koei Teruya, Ronald Yamanaka, Tony Foster, Testunosuke Yasuda, Ryoichi Onaga, Masataka Muramatsu, na Sensei Nantambu Camara Bomani ( Mwanzilishi wa Hekalu la kujilinda; Jundokan Tanzania), ni mwalimu wa kwanza kutoa wanafunzi watano wenye ngazi ya mkanda mweusi mwaka 1976 ni; Zebedayo Mapfumo Gamanya, Tola Sodoinde Malunga, Daudi Magoma Nyamuko Sarya, Abome Mabruki na Adombe Mabruki. Sensei Bomani alikuwa ni mwafunzi wa Eiichi Miyazato toka 1968 hadi kifo chake 1999. Hao wote ni walimu wa kuu duniani wa Jundokan Karate duniani na kupitia mafunzo chini ya Eiichi Miyazato sensei.
Sensei Rumadha Fundi pia at www.facebook.com/fundi.romi
No comments:
Post a Comment