ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 7, 2015

UZINDUZI WA TAWI LA BENKI YA DTB -KAHAMA

Mehboob Champsi, Mwenyekiti wa bodi, DTB, Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Bi. Nasim devji ambaye pia alizaliwa wa mji wa kahama, amesema benki hiyo ina matawi 110 na imepanga kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi na kwamba kwa hivi sasa inahudumia nchi za kenya, uganda burundi na Tanzania.
Bi Nasim devji Akitoa ngao kwa mfanyakazi wa DTB Bank
Meneja wa tawi la DTB Bank kahama tawila kahama Mercy Stephen akipokea ngao ya kuwa meneja wa kwanza kwa tawi la kahama Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Bi. Nasim devji
Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Bi. Nasim devji Akiwa na mama yake mzazi ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Bank hiyo sherbanu kurji
Wakipata chakula na wangeni walikwa
Mambo ya msosi wa SUB marine bana warembo
Meneja wa Hotel ya Sub Marine Baada ya kazi kubwa walijipongeza kwa kula na kunywa pamoja wache weeee DTB BANK hakunaga
Hili Ndiyo jengo jipya la Bank ya DTB Kahama 
Mgeni Rasm sherbanu kurji akilishwa keki na kaimu mkuu wa kituo cha polisi kahama Maduhu ambaye pia ni mama mzazi wa Nasim Devji wakati wa ufunguzi wa Bank hiyo
Baadhi ya wateja waliofika kufungua akauti zao mpya katika bank hiyo
Meneja wa tawi la Bank ya DTB Mercy stephen akibadilisha mawanzo na baadhi ya waandishi waliolikwa mwenye tishet nyeusi ni miliki wa malunde Blong mjini shinyanga 
Afisa Habari wa DTB Bank Bahati wakibadilisha mawanzo na wateja wao walialikwa katika ufunguzi huo.

KAHAMA
Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameombwa kujiwekea utaratibu wa kutunza fedha zao katika taasisi za kibenki ili kuziweka katika hali ya usalama zaidi ambazo zitawasaidia katika matumizi yao ya baadae.

Hayo yamesemwa na meneja wa benki ya Diamond Trust tawi la Kahama Mercy Stephen katika hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo wilayani Kahama na kusema kuwa wananchi wasiwe waoga kutumia taasisi za kifedha zinazowazunguka.

Mercy amewashukuru watu wote walioshiriki kufanikisha hafla hiyo ya uzinduzi wa Benki hiyo wilayani Kahama na kuwaomba watu wote kutumia fursa ya uwepo wa benki hiyo ambayo imejipanga kuwahudumia wananchi kulingana na uwezo wa vipato vyao.

Naye mtendaji mkuu wa Benki ya Diamond Trust hapa nchini Nasim Devji katika hotuba yake amesema benki hiyo itaendelea kujipanua ili huduma zake ziweze kuwafikia wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo kote nchini ili kuwainua kiuchumi.

Benki ya Diamond Trust inakuwa ni benki ya 10 ya kibiashara kufungua milango yake katika halmashauri ya mji wa Kahama na kuanza kutoa huduma za kibenki wilayani kahama ikiwalenga wafanyabiashara wa wadogo na wa kati.
Benki ya Diamond trust imepata ongezeko la faida ya asilimia 25 na kuwa sh. bilioni 20.09 tangu mwaka jana ikilinganishwa na pato la sh. bilioni 16.13 mwaka 2013 kufuatia kukua kwa mtandao wa matawi yake hapa nchini ambayo yanafikia 23.
Akisoma taarifa ya benki hiyo, wakati wa ufunguzi rasmi wa tawi la benki hiyo, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Mwenyekiti wa bodi ya DTB nchini, Mehboob Champsi, amesema mafanikio hayo yametokana na huduma nzuri zinazotolewa na benki hiyo hasa kwa kuwahudumia wafanyabiashara ndogo ndogo hapa nchini.

Kwa upande wake, Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Bi. Nasim devji ambaye pia ni alizaliwa wa mji wa kahama, alisema benki hiyo ina matawi 110 na imepanga kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi na kwamba kwa hivi sasa inahudumia nchi za kenya, uganda burundi na Tanzania.

Benki hiyo inatarajia kufungua matawi mengine katika mikoa ya Mwanza, Mara, singida na Kigoma.

Habari na picha kwa hisani ya Mohab Matukio

No comments: