ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 21, 2015

WATANZANIA WALIORUDISHWA TOKA YEMEN WAONGEA NA WANAHABARI


Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwarejesha nyumbani jumla ya Watanzania kumi na nane kutoka nchini Yemen kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo ya wenyewe kwa wenyewe.

Watanzania hao ambao wamewasili nchini leo kwa ndege ya shirika la emirates namba EK 725 wameishukuru serikali kutokana na jitihada za haraka zilizofanywa kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Oman na kufanikiwa kuwarejesha salama pasipo gharama zozote .

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Watanzania hao Bw. Sabri Abeid Almaghi ambaye alikua anafanya biashara nchini Yemen amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa namna ya pekee kwa kuwajali wananchi wake bila kujali wapo nchini au nje ya nchi na kutoa msaada kwa wakati.


“Tunaishukuru sana serikali yetu ya Tanzania kwa jinsi ambavyo wanajali wananchi wake bila kujali wapo ndani au nje ya nchi, kweli kama sio jitihada za ubalozi wetu pale mjini Muscat, sijui leo tungekua katika hali gani, tunaomba shukrani zetu mzifikishe kwa Rais Kikwete, Waziri Membe na wahusika wengine wote waliofanikisha kuturejesha nyumbani” alisema Mzee Saleh Mbaraka Jabri mmoja wa watanzania hao waliorejea kutoka Yemen.

Aidha, akizungumzia hali ya usalama ilivyo nchini Yemen, Bw. Almaghi amesema kuwa hali ni mbaya sana kufuatia mapigano ya anga yanayoendelea hivi sasa na muda wowote yataanza mapigano ya ardhini. Aidha amesema kuwa kufuatia hali hiyo huduma zote za kijamii pamoja na biashara zimesimama.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea watanzania hao Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini Bi. Mindi Kasiga amesema mpaka hivi sasa watanzania ambao wamesharejeshwa nchini kutoka Yemen ni 23, kati ya Watanzania 69 ambao wamejiandikisha na jitihada zinaendelea.

“Awamu ya kwanza ya Watanzania waliorejeshwa na serikali kutoka nchini Yemen ni familia moja ya watu watano ambao walirudi wiki chache zilizopita” alimalizia Bi. Mindi Kasiga.

Hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ilitangaza kuwarejesha nchini Watanzania waliopo Yemen kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo

2 comments:

Anonymous said...

Ninyi waandishi mnavyowahoji watu mnahitaji kuwa professional. Angalia huyo dada anayeropoka huku ameacha microphone on, sauti yake inatoka background na huyo mwandishi mwanaume anayeongea naye sauti zao zinapiga kelele kabla hawajaanza kuwahoji hao abiria. Pia wakati wa kuwahoji haisikiki sauti vizuri zaidi ya sauti ya kukwaruza kwaruza. Jamani hamuwaoni wenzenu wa BBC,CNN, CCTV, NTV au KBC wanavyoendesha mahojiano yao ki-professionally sio ninyi mnaropoka ropoka tu.

Anicetus said...

Wanafunzi ambao Tanzania iliwapeleka nchi za nche kusoma ( cultural exchange scholarships) nche wanapata taabu sana. Hao wanafunzi wakimaliza masomo, serikali ya Tanzania haiwafutalii na haiwapi msaada wa kuwarudisha nyumbani kundelesha nchi yao. Wengine wamefariki kwa kukosa msaada wa serikali- gharamam za matibabu- psychological problems and others.

Kila president wa Tanzania aneakuja huku America pamoja na vionngozi wake wanaambiwa tatizo hilo. Huu ni wakati wa Tanzania kuanagalia watanzania wote na sio kundi moja tu.

For further information write to : temba@tembausa.oom, or call 347 489 6532