DONGO! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba.
Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki.
Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya.
“Hamna jipya waache waendelee kumpigia kampeni (Kiba) lakini mimi nafanya muziki wangu, mashabiki wanafahamu. Kwa hao watoto wa kike, hakuna kipya kwangu si kimuziki hata maisha yao binafsi.
“Wema namjua vizuri, Jokate ndiyo usiseme. Mwache huyo Kiba aendelee kula makombo kwa Jokate kama ameamua kipita njia nilizopita si mbaya, inaruhusiwa,” alisema Diamond.
Jitihada za kumpata Jokate ili aweze kufunguka kuwa anajisikiaje kuitwa makombo na Diamond hazikuzaa matuda kufuatia simu yake kuita bila kupokewa, jitihada zinaendelea.
7 comments:
Kuna msemo unasema halua haina makombo hujawahi kuusikia dai halafu acha kutukana mama zako ukimtukana mwanamke yeyote ni kama umetusi mzee wako maana hatuna tufauti jitahidi Kuwait muungwana punguza ushamba kidogo
yeye domondo ndo anakula makombo yaliochacha kabisa..
Duh Jamal Ana kejeli, na yeye si anakula makombo zaidi. Zari keshtotoleshwa watoto wa watatu. Angenyamaza tu! Afanye kazi yake! Kuliko kutusi watu.
Tena makombo yalio chacha ya Ivan,
Makombo yalio chacha ya watoto watatu.
Wacha Ushamba ,angalia kauli zako siku izi umezidi.
si mnaona sasa jinsi mnavyo dharaulika kujidai masuper star,sijui wazuri watoto wa mujini,sexy figure na legs kila leo kutuonyesha makalio yenu na mkishikwa halafu mnatupwa kule.
amkeni watoto wakike acheni ujinga ujinga wakujiona wazuri bila ya elimu na kipato.itakula kwenu
Watch your mouth and control your temper, you are public figure kaka. Kama JoJo makombo Zari atakuwa nani?
Dai mdomo uliponza kichwa. Dai anajua maana ya makombo? Bora makombo ya Jokate njia haijapitisha watoto. Sasa mwenzangu namie Dai makombo unayokula wewe imepitisha vichwa vitatu. Maana kama ni makombo mwenzetu Dai unakula makombo yaliochacha tena hayafai hata kuliwa.
Post a Comment