Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na baadhi ya viongozi Jumuiya ya Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA Zanzibar), walipofika nyumbani kwake Mbweni kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mratibu wa TAMWA Zanzibar bi Mzuri Issa nyumbani kwake Mbweni.
Mratibu wa TAMWA Zanzibar bi Mzuri Issa akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni.
Mjumbe wa TAMWA Zanzibar bi Fatma Said, akikabidhi kabrasha la TAMWA kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya mazungumzo yao nyumbani kwake Mbweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TAMWA Zanzibar waliofika nyumbani kwake Mbweni kwa mazungumzo.(Picha na Salmin Said, OMKR).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar itaweza kushinda vita dhidi ya udhalilishwaji wanawake na watoto iwapo kutakuwa na nguvu ya pamoja kati ya Serikali, jumuiya za kiraia na jamii nzima katika kuvitokomeza.
Maalim Seif amesema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar, waliofanya naye mazungumzo huko nyumbani kwake Mbweni mjini Unguja, kuhusiana na shughuli wanazozifanya.
Amesema mbinu muafaka ya kutokomeza vitendo hivyo ni kufanyika utafiti wa kina ili baadaye wadu wote wakiwemo Polisi, Mahkama, viongozi wa dini, wana jamii na Serikali kuwekewa mkakati maalum katika kufanikisha wajibu wa kila upande.
Maalim Seif amesema hali ya udhalilishwaji wanawake na watoto Zanzibar imefikia katika kiwango cha kutisha na nilizima hatua zinazochukuliwa na taasisi mbali mbali, ikiwemo TAMWA Zanzibar ziungwe mkono kwa nguvu zote.
Makamu wa Kwanza wa Rais amekipongeza Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar kutokana na kazi nzuri ya kupigiwa mfano yanayoifanya kuelimisha jamii kukomesha vitendo vya udhalilishwaji wanawwake na watoto.
“Kuishawishi jamii na hasa wanaume waachane vitendo hivi si kazi rahisi, lakini nyinyi mnaifanya kwa ufanisi, nadhani hatua mliyofikia sasa ni ya mafanikio makubwa”, alisema Makamu wa Kwanza wa Rais.
Naye Mratibu wa TAMWA Zanzibar, Mzuri Issa amesema mbali na kupiga vita vitendo vya udhalilishwaji, Jumuiya hiyo inaendelea na juhudi za kuwajengea uwezo wanawake wa Zanzibar katika maeneo tafauti, ikiwemo kuwawezesha kushika nafasi za maamuzi, ikiwemo Ubunge na Uwakilishi.
Amesema mbali na wanawake kuonesha uwezo mkubwa katika kusimamia majukumu yapo wanaposhika nyadhifa mbali mbali, lakini wamekuwa wakipambana na vikwazo vigumu wanapoamua kuwania nafasi za kisiasa kupitia vyama.
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wanawake (UN Women), Ali Sultan akizungumza katika hafla hiyo amesema miongoni mwa hatua wanazozichukua ni kuwapa ujasiri na kuwaondolea hofu wanawake kwa azma ya kuwawezesha kuwania nafasi mbali mbali za kisiasa kupitia vyama vyao.
Khamis Haji, OMKR
3 comments:
hana lake jambo, hana lolote misisiyemu ndo ilivyo.weupeeee kama unga wa ndwerwe
maalim vipi yakhee unapeana mikono na wanawake,dini yako inaruhusu wanawake unao weza kuwaowa kupeana mikono?vipi yakhee?
wewe mwenye comment ya 11:32 kama huna cha kuongea uwe unakaa kimya sasa asipeane mikono na mwanamke ulitaka apeane mikono na gay kama wewe? hiyo dini gani inayokataza mtu kupeana mikono na mwanamke? umejifunza wapi uislam wako? ndio nyinyi mnaokurupuka kuongeza maneno katika dini yetu takatifu ambayo hayapo,ni kitabu kipi cha mtume wetu kilisema usipeane mikono na wanawake? na hao wanawake basi maalim amekua mnyama anaoa mpaka mama yako? umekalia kutafuta uchonganishi wa amani binadamu wametulia wanaishi kwa amani kama hivi wanatembeleana na kucheka wewe na mastress yako unaleta mistiri ya dini yako ya kujitungia, tuondolee laana zako hapa kwendraaaa
Post a Comment