Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiwajadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR), Balozi Mwanaidi Maajar huku Mkuu wa Chuo hicho Balozi Mohammed Maundi akisiskiliza wakati viongozi hao wakisubiri kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi alipotembelea Chuoni hapo leo tarehe 18 Mei, 2015 wakati akiendelea na ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini. Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini, Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1978 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Maundi alipotembelea Chuoni hapo wakati wa ziara yake hapa nchini
Juu na Chini: Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Wahadhiri, Wanafunzi na Wageni mbalimbali alipotembelea Chuo cha Diplomasia (CFR)
Wajumbe wakifurahia jambo wakati Rais Nyusi (hayupo pichani) alipozungumza nao
Mhe. Rais Nyusi akifurahia zawadi ya picha ya kuchora inayowaonesha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel aliyozawadiwa alipotembelea Chuo cha Diplomasia
Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Msumbiji pamoja na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia (wa kwanza kushoto) ambaye ni Waziri anayeongozana nae kwenye ziara hii.
Mhe. Rais Nyusi akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia
Rais Nyusi akiangalia bango linalosomeka
"CHUO HIKI KILIKUWA CHUO CHA ELIMU YA JUU KWA WAPIGANIA UHURU WA AFRIKA" ikiwa ni jina la awali kabla Chuo cha Diplomasia hakijaanzishwa.
Mhe. Rais Nyusi akiangalia Jiwe la Msingi la kuanzishwa kwa Chuo hicho
......Rais Nyusi alipozugumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini
Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akifurahia kikundi cha ngoma cha Raia kutoka Msumbiji wanaoishi hapa nchini alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kuzungumza nao.
Sehemu ya umati wa Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa nchini wakimpokea kwa shangwe Rais Nyusi alipokutana na kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini
Mhe. Rais Nyusi akizungumza na Raia wa Msumbiji waishio hapa nchini (hawapo pichani)
Mhe. Rais Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa Raia wa Msumbiji wanaoishi hapa nchini
......Rais Nyusi aliposhiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji
Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kushiriki na kufungua rasmi Kongamano la kukuza Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji. Wakati wa Kongamano hilo mada mbalimbali kuhusu fursa za uwekezaji baina ya nchi hizi mbili zilitolewa.
Mhe. Rais Nyusi kwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Christopher Chiza (kushoto) wakifuatilia mada za uwekezaji zilizowasilishwa wakati wa kongamano la kukuza uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji
Wajumbe waliohudhuria kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment