Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Jijini Dar es Salaam,ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kitaifa ya siku tatu nchini Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein akiwa ameongozana na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika Zanzibar leo tarehe 18 Mei, 2015.
Rais Shein akiwa na Rais Nyusi kwenye Jukwaa Maalum wakati nyimbo za Taifa zikipigwa kwa heshima ya Rais Nyusi.
Rais wa Msumbiji Mhe.Nyusi akikagua Gwaride la Heshima wakati wa mapokezi yake.
Rais wa Msumbiji, Mhe.Nyusi pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe.Dr.Shein wakifurahia burudani ya kikundi cha ngoma wakati wa mapokezi hayo huku Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad (kulia kwa Rais Shein) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Balozi Seif Ali Iddi (kulia) wakifurahia pia burudani hiyo.
Rais Nyusi na Rais Shein wakiteta jambo wakati wakiangalia burudani ya ngoma za asili.
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo |
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt.Ali Mohamed Shein akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji pale alipomkaribisha Ikulu kwa mazungumzo.
.....Kuelekea Hotelini
Halaiki ya Wanafunzi waliokuwa wamejipanga barabarani kusherehesha mapokezi ya Rais wa Msumbiji Visiwani Zanzibar.
Rais wa Msumbiji akiangalia mmoja wa watumbuizaji anavyopuliza kifaa chake kwa ustadi mkubwa huku akiwa amejilaza chini wakati Rais huyo akiwasili hotelini kwake
Picha na Reuben Mchome
No comments:
Post a Comment