Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest
Mangu, mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano
ya Dharura cha Polisi, iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha
Polisi,jijini Dar es salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Katikati (mwenye tai) ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Makame Mbarawa ambaye pia alihudhuria hafla hiyo.kULIA NI Kamishna wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es
salaam, Suleiman Kova,
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia), akiteta jambo na Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu, katika hafla ya uzinduzi wa
Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya Kituo
cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akihutubia katika hafla ya
uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi iliyofanyika katika
viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam. Waziri Chikawe
alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini(IGP), Ernest
Mangu, akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, mara
baada ya kufungua kituo cha Mawasiliano
ya Dharula cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha kati cha
Polisi,jijini Dar es salaam.Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika hafla
hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (wa nne kutoka kulia mstari wa
kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kulia – mstari wa mbele),
viongozi mbalimbali wa jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP) Ernest Mangu( watano kutoka kulia) na Wawakilishi mbalimbali kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha
Mawasiliano ya Dharura cha Polisi uliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati
cha Polisi,jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment