ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 8, 2015

JANUARI MAKAMBA AMFUNIKA LOWASA

NAIBU Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba ambaye ni mmoja wa makada wa CCM waliotangaza nia ya kuwania kuteuliwa kuwania Urais, ameibuka na ubunifu wa kisasa katika namna ya kutangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, kitu ambacho endapo kitafanikiwa atakuwa amemfunika Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa ndiye gumzo miongoni mwa makada waliojitokeza.
Edward Lowassa.Januari, ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, mzee Yussuf Makamba, jana katika Ukumbi wa Mlimani City, alitegemewa kutangaza nia ya kutaka nafasi hiyo ya juu kisiasa nchini, katika tukio ambalo lingeonekana pia katika kumbi mbalimbali nchi nzima zilizokuwa zimeandaliwa na kujaza watu waliomsikiliza na kuuliza maswali ya moja kwa moja.
Januari MakambaAkizungumzia kuhusu suala hilo, Makamba alisema kumbi katika mikoa mbalimbali nchini zilikuwa zimeandaliwa, ambazo zingefungwa skrini kubwa ambayo watu waliomo wangeweza kumuuliza maswali Makamba akiwa Mlimani City jijini Dar es Salaam, teknolojia ambayo itakuwa inatumiwa kwa mara ya kwanza na mwanasiasa nchini tangu Tanzania ipate uhuru wake.
Licha ya kuonekana katika skrini hizo, watu wangepa fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo kutoka popote walipo.
Gazeti hili lilikuwa limeshakwenda mitamboni kabla mwanasiasa huyo hajatangaza nia yake.
Kabla ya ubunifu huo, Lowassa alikuwa akishikilia rekodi ya tukio lake la kutangaza nia kwa kujaza watu wengi uwanjani huku maelfu wakifuatilia katika vituo vya televisheni tukio hilo lililofanyika Mei 30, jijini Arusha.

3 comments:

Anonymous said...

Hongereni sana Mr. January Makamba na Mr. Edward Lowasa. Ili CCM wajihakikishie ushindi wa nguvu zidi ya UKAWA watakiwa wamteue Dr. John Magufuli au Prof. Mark Mwandosya. Ni lazima CCM wasome alama za nyakati "chama kwanza mtu baadae".

Anonymous said...

AND THEN WHAT HAPPENED? NI VIZURI KUMALIZIA STORY CHALII ALIMFUNIKA LOWASSA AU LAA???

Anonymous said...

Kimsingi hizi mbio zote dhumuni lake ni moja tu, yaani kupata urais. Sasa basi si January wala Lowasa au mwingine yeyote katika hao wote waliotangaza nia na kuchukua fomu mwenye uwezo wa kuwashinda UKAWA, isipokuwa ni Magufuli au Mwandosya, labda Membe kidogo sana. Ila CCM wakikosea na kutazama ushabiki, watakufa kifo cha mende. Kitu unachotakiwa kufahamu bw. Ano. 8.43am ni kuwa kuna watu walipata fedha nyingi bila kutumia jasho ndio hizo wanazochezea. Wengine walipata kupitia Richmond, Esscro, wengine kupitia baba zao, sasa hiyo haina manufaa kwa taifa, ila inaweza kuwagharimu sana kama chama.