ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 7, 2015

SIR. GEORGE KAHAMA AMBARIKI MH. MEMBE KUWANIA URAIS WA TANZANIA


Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto waliokaa), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana. Wengeni (kutoka kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Adelina Gefi na Mke wa Waziri Membe, mama Dorcas Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), akimpongeza Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama baada ya Mzee Kahama kuhutubia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Mheshimiwa Membe alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.

Mama Dorcas Membe mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akimpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa baada ya kuhutubia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoani humo jana, wakati Mheshimiwa Membe (katikati), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.

5 comments:

Anonymous said...

Kwanza niseme kuwa siko affiliated na mgombea yoyote au chama chochote.Lakini hotuba ya Membe imeni disappoint sana,nilitegemea baada ya kuwa waziri kwa mambo ya nje kwa takribani miaka 9 angekuwa amejenga uwezo wa kupanga hoja zilizo na mashiko lkn he did just to the contrary. .

Anonymous said...

Member hawezi ku-deliver na hajawahi ku-deliver. Sio lazima tung'ang'anie uongozi ilihali historia inaonyesha hatuwezi.

Anonymous said...

Wengi wao hawa hamna kitu kabisa. Wanapeana kazi kwa mjuano, wala siyo kwa kujua kazi. It's a disaster. Yule mheshimiwa sana, Lowassa ndiyo hamnazo mwingine

Anonymous said...

urahisi umekuwa rahisi sana tanzanaia duuu aiseee.

watia nia katika ubora wao haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Anonymous said...

Kingunge alilaumiwa na watu alipo muunga mkono Lowasa, sioni watu wakisema lolote kuhusu Kahama kuunga mkono membe. Haki iko wapi hapa?