ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 28, 2015

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA MKOANI IRINGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo . Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za Kilolo na Mufindi. Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa katika mikoa aliyokwishafanya ziara kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima, wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Iringa kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiwasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub huku Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akishuhudia.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub (kushoto) akitoa taarifa migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo na utekelezaji wake.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub akitoa taarifa migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo na utekelezaji wake.
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Iringa wakifuatilia kwa kina taarifa ya migogoro iliyokuwa ikisomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub (hayupo pichani).
Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi akizungumza katika kikao hicho kilichowashirikisha watendaji wa mkoa wa Iringa.
Ofisi za NHC mkoa wa Iringa kama zinavyoonekana leo hii, ambapo Waziri Lukuvi alitembelea na kuagiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa linaboresha mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa linajenga nyumba bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiri ili liweze kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ili ziwanufaishe wananchi wengi zaidi.
Meneja wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo akitoa taarifa ya utendaji ya NHC mkoa wa Iringa kwa Waziri Lukuvi wakati Waziri huyo alipotembelea Shirika hilo leo asubuhi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akifutilia taarifa hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa mkoa wa Iringa wakifuatilia taarifa ya utendaji wa Shirika iliyokuwa ikitolewa na Meneja wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo (hayuko pichani).

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akizungumza na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na wale wa sekta ya ardhi na Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa ambapo alisisitiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa linaboresha mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa linajenga nyumba bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiri ili liweze kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ili ziwanufaishe wananchi wengi zaidi..
Baadhi ya watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa mkoa wa Iringa wakifuatilia taarifa ya utendaji wa Shirika iliyokuwa ikitolewa na Meneja wa NHC mkoa wa Iringa, Humphrey Kishimbo (hayuko pichani).
Ofisi za NHC mkoa wa Iringa kama zinavyoonekana leo hii, ambapo Waziri Lukuvi alitembelea na kuagiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa linaboresha mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa linajenga nyumba bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiri ili liweze kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ili ziwanufaishe wananchi wengi zaidi.
Waziri Lukuvi akikagua mafaili yaliyopo katika masjala ya Ardhi ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ili kujionea utendaji wa wanfyakazi wa kitengo cha ardhi.
Waziri Lukuvi akionyeshwa Master Plan ya Manispaa ya Iringa ambayo iko katika mchakato wa kukamilika kwaajili ya kuanza kutumika kuupanga vyema mkoa huo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Iringa uharakishe kupima ardhi ya wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri Lukuvi aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya Iringa.

No comments: