Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan ametoa wito wa kutunza mali asili na mazingira kwa sababu
ni urithi kwa vizazi vijavyo. Aliongea hayo alipokuwa akifungua mkutano wa
Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa idadi
ya watu duniani inazidi kuongezeka hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuacha
kukata miti hovyo, kuacha kuchoma misitu na vitu vyote vinavyosababisha
uharibifu wa mazingira kwa sababu upo uhusiano wa karibu sana kati ya umaskini
na uharibifu wa mazingira. 'Uharibifu wa mazingira huongoza kusababisha
umaskini' alisema Bi Samia.
Aidha alisisitiza kuwa matokeo yataonekana iwapo maazimio yaliyopendekezwa katika Azimio la
Gaborone yatatiliwa maanani. Mkutano huo wa
Wadau wa Azimio la Gaborone umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa
kushirikiana na Serikali ya Botswana. Wadau mbalimbali wa mambo ya mazingira
kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamehudhuria Mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone juu ya utunzaji Mazingira jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada katika Mkutano huo Bwana Carlos Manuel Rodriguez akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Sehemu ya Wadau wa Mkuatano huo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano huo.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wadau waliohudhuria Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment